IDADI YA WANAWAKE KATIKA KINYANG'ANYIRO CHA URAIS YAFIKIA WANNE, DKT.ASHA MIGIRO ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA URAIS WA TANZANIA

CCM imepanga kuanzia mwezi huu hadi Julai 2 kuwa ni muda wa makada wake kuchukua na kurudisha fomu kabla ya vikao vya juu vya chama hicho kukutana kuanziaJulai 12 kuchuja wagombea na baadaye kumpata mmoja atakayesimama kwenye Uchaguzi Mkuu kupambana na wa vyama vingine.

Baada ya makada wa CCM kutangaza nia na hatimaye kuchukua fomu za kugombea urais ikiwa imefikia idadi ya makada 34 wameshachukua fomu, sasa leo june 15 waziri wa katibu na sheria Dkt. Asha Migiro amekuwa mwanamke wa nne kutoka kwenye chama hicho kuchukua fomu ya kugombea za ridhaa.
Akizungumza kupitia TBC1 alisema ‘Kwanza nakishukuru chama cha mapinduzi kwa kuweka mazingira ya kutufanya wengi tujitokeze mara baada ya kufungua pazia la kusaka wale ambao watapata ridhaa ya chama cha Mapinduzi...”
Previous
Next Post »