PICHA 5 ZA RAPPER GUCCI MANE AKIWA KWENYE PINGU, PIA KUHUSU KUMPIGA MWANAJESHI


Rapper Gucci Mane ni miongoni mwa mastaa wa muziki walioingia kwenye headlines mara nyingi kutokana na kesi za ugomvi ambapo wakati huu ana kesi ya kumpiga mwanajeshi kichwani kwa kutumia chupa ya champagne mwezi huu.
Ishu yenyewe ilitokea wakati mwanajeshi huyo wa Marekani ambae ni shabiki wa Gucci alikua akisherehekea siku yake ya kuzaliwa ndipo akaamua kumfata rapper huyo kwenye sehemu ya V.I.P kwenye club ya usiku ya Harlem huko Atlanta na kuomba kupiga nae picha, ilikua tofauti na matarajio kwa sababu Gucci hakumjibu vizuri na pamoja na hilo akamgipa chupa iliyosababisha akimbizwe hospitali na kushonwa nyuzi kumi.
Baada ya hii ishu ya mwanajeshi, kuna jamaa mwingine anaitwa TJ alijitokeza na kusema na yeye alipigwa na Gucci Mane siku mbili kabla ya kumpiga James, alipata kipigo baada ya kujaribu kumsalimia Gucci muda mfupi baada ya kumaliza show kwenye stage.
.
.
Mwaka 2001 Gucci alitumikia siku 90 jela kutokana na kukutwa na dawa za kulevya, 2005 alifungwa miezi sita, mwaka 2009 alifungwa jela kwa mwaka mmoja, 2011 alifungwa miezi 6 baada ya kukiri kumfanyia fujo mwanamke mmoja Georgia.
.
Previous
Next Post »