Rais wa Sudan ameondoka Afrika Kusini


Rais Omar al Bashir wa Sudan
Rais Omar al Bashir wa Sudan ameondoka nchini Afrika Kusini.
Rais Bashir ameondoka akiandamana na waziri wa maswala ya kigeni wa Sudan huku ikiahidiwa kuwa watazungumza na waandishi wa habari pindi watakapotua mjini Khartoum.
Mwandishi wa BBC aliyeko Afrika Kusini Nomsa Maseko, anasema kuwa ndege ya rais al Bashir ilijazwa mafuta jana usiku na kuwekwa mstari wa mbele tayari kabisa kuondoka katika uwanja wa ndege wa kijeshi.

Rais Bashir amekuwa nchini Afrika kusini kuhudhuria kikao cha viongozi wa Umoja wa Afrika mjini Johannesburg.
Rais Bashir ameondoka licha ya kuwepo amri ya mahakama ya kumzuia kuondoka nchini humo hadi kesi dhidi yake itakaposikizwa.
Mahakama hiyo ilikuwa inapaswa kuamua ikiwa Bwana al-Bashir atakabidhiwa kwenye mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ICC yenye makao yake mjini Hague Uholanzi ilikukabiliana na mashtaka ya uhalifu wa kivita na mauaji yahalaiki yanayomkabili .
Majaji watatu walikuwa wanasikiza kesi hiyo rais Bashir alipopuzilia mbali amri hiyo na kuondoka.
CHANZO BBC
Previous
Next Post »