Shirika la Umoja wa Mataifa
la Idadi ya Watu (UNFPA) Tanzania kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango, wameandaa warsha kwa ajili ya kuhamasisha na kuwajengea uwezo watumishi
wa Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhusu kujumuisha masuala ya vijana
katika mipango ya Mkoa na wilaya.
Warsha hiyo inafanyika
katika vituo vya Mwanza na Musoma. Katika kituo cha Musoma warsha inafanyika
katika ukumbi wa Afrilux Hotel tarehe 11 na 12 Juni 2015. Kituo hiki kinajumuisha
Sekretarieti ya Mkoa na Halmashauri za mkoa wa Mara na Simiyu.
EmoticonEmoticon