TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 11.05.2015.
WATU KUMI NA TANO WAJERUHIWA KATIKA
AJALI ILIYOHUSISHA MAGARI MATATU KATIKA BARABARA YA NJOMBE/MBEYA.
WATU KUMI NA TANO WAJERUHIWA KATIKA AJALI ILIYOHUSISHA
BASI LA ABIRIA MALI YA KAMPUNI YA TAQWA LENYE NAMBA ZA USAJILI T.791 BZR AINA YA NISSAN LILILOKUWA
LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE SALUMU
SELEMANI (45) MKAZI WA D’SALAAM KULIGONGA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.778 CAN ISUZU FTR LIKIENDESHWA NA
DEREVA AITWAYE EDWIN LUYENGA (40) NA
KISHA KUGONGA KWA NYUMA GARI T.565
CVB/T.836 BBC AINA YA MAN LILILOKUWA LIMEHARIBIKA NA KUEGESHWA.
AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 10.05.2015 MAJIRA YA SAA
20:10 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA KAPYO, KATA YA MAHONGOLE, TARAFA YA
ILONGO, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/NJOMBE.
MAJERUHI KATIKA AJALI HIYO NI WANAUME TISA [09] NA WANAWAKE
SITA [06] WALIFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1.
APAMAT UMUYU (41) MKONGO 2. SALUMU
RASHIDI (29) MKAZI WA DSM 3. JUMA
RAJABU (34) MKAZI WA ZANZIBAR 4.
ANNA MISIKITA (36) MKONGO 5. DAVID
MTACHI (43) MKAZI WA DSM 6. GROLI
AMANI (41) MKAZI WA DSM 7. KELVIN
JORDAN (39) MKAZI WA DSM 8. WAZIRI
OMARY (35) MKAZI WA DSM 9. MCHEMBE
GEORGE (35) MKAZI WA MWANZA.
MAJERUHI WENGINE NI 10. LIKA ILUNGA (47) MKAZI WA KONGO 11. MAJARIWA RAMADHANI (51) MKAZI WA KAGERA 12. ADELA MUTOMBA (46) MKAZI WA KONGO 13. MUDY ABDALLAH (43) MKAZI BUKOBA 14. NASORO MKAZI WA TANGA, MAJERUHI MMOJA MWANAMKE AMETIBIWA NA
KURUHUSIWA NA WENGINE 14 WAMELAZWA
HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA DEREVA WA BASI
AMBAYE AMEKAMATWA.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI NYIGESA R. WANKYO
ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI
PAMOJA NA KUFUATA SHERIA/KANUNI/ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI
ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
Imesainiwa na:
[NYIGESA R. WANKYO – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon