MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.
Sim no, 0755683295/Watsap, Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala, Email@yusuphngahala@gmail.com, Instagram @mwalim_yuu.
Tulipoishia, Au nao umeporwa na mwanaharamu yule? Kama umeporwa nimekwisha! Uko wapi? Nilimwuliza maswali mfululizo kisha nikatulia kidogo! Nikasema nijibu basi. Ndipo kwa sauti ya kulia lia akajibu kuwa____Enda nayo sasa............ Niko nao brother, huu hapa mfukoni. Basi kusikia vile roho ikatulia nikawasha gari na kumkimbiza hospitali. Tulifika kule nikakutana na yule mkuu akiwa anamsubiri mke wake akae vizuri kiafya. Nilimsalimu alipoona mguu wa Oscar akasema kwa uzoefu ile ni sumu ya mifupa hivyo tukichelewa anaweza akapooza. Maneno yale yalinitisha kiasi basi nikamwita dakitari ambaye alikuja na kuanza kumhudumia.
Nilirudi kuongea na mkuu mpya wa kituo pale nje. Nikamweleza jinsi gani majambazi wanalisumbua taia letu. Alinipongeza sana kwa ujasiri. Kisha akasema ipo siku atanirudisha kazini niwe mvunilivu. Nilifurahi kiasi lakini nikamwambia mpaka nikamilishe kuuweka ukweli wa Zabroni na Peris na kundi lake hadharani ndipo nitarudi na kuaa sare za jeshi la polisi. Mda ukasonga huku na kusogea. Taarifa ikaja kua mgonjwa ameshatolewa sumu hivyo naweza kuondoka naye. Nilimfuata nikamsaidia kutembea mpaka nje. Nikamfikisha kwenye gari na kumpakia kisha tukaondoka zetu.
Baada ya kufika nyumbani Oscar alihitaji kupumzika. Nikamtoa na kumlaza ndani. Kisha nikamwambia kabla hujalala nipe mkanda. Akainiza mkono mfukoni kisha akasema bro nahisi nimeangusha kwenye gai ndani. Nikamjibu sawa kisha nikatoka kuangalia. Wakati nafungua mlango wa upande wa kulia upande wa kushoto nilimwaona mwanamke naye akifungua mlango akitoka katika gari yangu. Nikamwuliza we nani? Hakujibu nikamwuliza tena ulikua uatafuta nini kwenye gari yangu. Hakujibu ila akainua mkono na kunionyesha ule mkanda.
Hasira ikanipanda nikajikuta nimeruka kwa nguvu juu ya gari na kumpiga ngumi kichwani. Alianguka na mimi nikaanguka kwa bahati mbaya alikua mwepesi kuliko mimi aliinuka araka zaidi. Akaanza kukuimbia niliinuka na kumfuata nyuma. Nilikua na hasira sana. Alijitahidi kukimbia lakini wapi. Nilimkuta nikamsukuma na teke la haja akaangukia uso. Kisha mimi nikatua juu yake nikamkunja shingo kli nimnyonge ile naanza kuvuta shingo nilishitukia nachomwa na kisu mgongoni. Aumivu makali yakanifanya niachie na kugeuka kuona kuna nini. Ile ilimpa mwanya akaniinua kwa nguvu nikaanguka kisha akanipiga teke mabegani. Nikachowa na kisu tena. Kumbe viatu vyake vilikua na visu.
Maumivu yaliongezeka kisha yule dada akawa anaondoka akitembea kwa maringo. Niliumia sana kikweli. Alitokomea zake huku mimi nikikosa msaada na nikawa kama nisiyejua la kufanaya. Nilijaribu kunuka nikajiweza na kuamua kujikongoja mpaka nyumbani. Lakini wakati nafika nyumbani ile naingia nilimwona mtu akiwa kwenye kitanda alicholala Oscar nikajikaza na kumfuata kwa nguvu za kujilazimisha. Ile namfikia nilimwona ni Zabroni aliinuka na kunichoma sindano kisha akasema hebu pumzika tukafanye kazi yetu.
Baada ya kusikia maneno yale sikujua nini kilijiri. Mpaka hapo nilipokuja kushtuka ikiwa ni mida ya jioni. Niligundua hilo baada ya kuangalia saa. Iikua saa 12:45 nilikua nimelala singizi mzito. Oscar naye alikua bado kalala. Nikatoka nje nikajinyoosha na kunywa maji kisha nikarudi ndani nimwamshe Oscar. Nikachukua simu ili niangalie kama kuna mtu kanitafuta. Ndipo nikakutana na "missed call" za yule mkuu wa kituo zilikua 25. Nikahisi kuna tatizo nikampigia ndipo alipopokea nikasikia taarifa mbaya haswaa.
Alisema kuna kundi la majambazi walikua sita wamevamia vituo vinne vya polisi pale jijini Dar es salaam. Wameua askari wengi na kupora silaha za jeshi zote na pia walichoma vituo hivyo ili kama kuna taarifa zao ziungue. Habari ile ilinishtua sana. Kisha nikamwuliza kwasasa mko wapi mkuu. Ak anijibu ya kua wana kikao na wizara ya ulinzi na usalama. Nikawauliza mmefikia wapi? Akajibu hapa tuko na vyombo vya habari tunatolea maelezo. Nilitamani sana kwenda lakini ni hiyohiyo wizara kupitia waziri wake ndo nilisimamishwa kazi. Niliamua kukaa kimya na kutulia.
Nilimwamsha Oscar naye akashtuka kwa kushangaa ni usingizi gani alilala? Wakati tunaongea simu yangu ikaita nilipopokea nikasikia Afande Yuu unahitajika ofisini sasa hivi fanya haraka. Alikua ni mkuu wa kituo yule mpya. Askari inaidi kuwa tayari mda wowote. Ilinibidi nianze safari nilifika kituoni pale na kukuta maiti za maaskari zimezagaa pale nje mithili ya karanga zilizomwagika bila ushirikiano. Sikujali hilo nikaingia kwenye ukumbi maana kituo kilikua kimechomwa moto.
Baada ya kufika na kuwakuta kuna baadhi ya maafande pale wakaanza kushangilia. Nilkaribishwa na kuambiwa umeitwa kwa sababu kwasasa taifa linakuhitaji zaidi ya ufikiriavyo. Tunakupa jukumu la kuandaa vikosi na muhakikishe mnawatia nguvuni majambazi ndani ya wiki moja hii ni amri siyo ombi. Hivyo ndivyo walimaliza kuongea na kuinuka kisha kutuacha sisi pale kwa kua ilikua tayari ilikua usiku nijawaomba vijana wangu wajiandae kwaajili ya mapambano. Nikawaamuru pia kuzipeleka mochwari maiti zile usiku ule ule.
Nikatoka sasa kurudi nyumbani. Nilipofika nyumbani kwangu nilikuta taa zote mpaka ya chumbani kwangu inawaka. Sikujua ni nini kwani Oscar hakuwahi ingia chumbani kwangu. Wakati nafika mlangoni nikakutana na Oscar akiwa kalala huku kama aliyekua akiugulia maumivu. Nikamwuliza nini akajibu kuna mtu ndani. Nikajihami kisha nikaingia kumtafuta. Alikua mwanamke yule alikimbia siku ile aliponiumiza na visu. Nilimrukia kwa kasi. Na kumtwisha ngumi. Alichomo bastora na kunielekezea nikainua mikono kisha nikawa namsogelea. Alipoongea akisema tulia hapohapo ile sauti ilikua ya Peris kabsaa. Hali ile ilinifanya nitake kujua zaidi nikawa nazidi kumsogelea. Mara mlio wa risasi ukasikika Paaaaaaa!!!!!!!!______________
EmoticonEmoticon