MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.
Sim no,0755683295/Watsap, Fb.com/Mwalim Yusuph Abel Ng'ahala. Email@yusuphngahala@gmail.com, Instagram @mwalim_yuu.
SEHEMU YA 24.
Tulipoishia Nikasimama nje mara nesi akawa natoka. Tukakutana mlangoni. Haa hakuwa nesi niliyemtarajia bali alikua ni Peris amevalia mavazi ya manesi. Peris mke wangu alishtuka kiasi kisha___Songa nayo.............Akageuka mbele na kuanza kukimbia. Nilimkimbiza kwa nyuma kwa bahati mbaya yeye alikua ameshajua ramani ya ile hospitali. Alifika kwenye ukuta na kuruka kwa nje. Nilipruka sikumwona tena nilijilaumu sana nikatamani hata ningepiga kelele pale hospitalini lakini lile ni eneo la watu wagonjwa ningesumbua watu. Nikaamua kurudi wodini kumwangalia yule kijana. Wakati nafika nilimwona yule kijana anadalili zote ambazo mimi nilikua nazo nilipochomwa sindano ya sumu na Zabroni Makweka.
Nikatoka mbio hadi kwa daktari nikamwita. Alipokuja na kumwona akaamuru kuongezewa damu haraka. Kisha akamchoma sindano fulani. Baada ya masaa kama 13 hivi kupita yule kijana akazinduka. Alikua akihisi maumivu. Kwakua tayari usalama wake ulikua mdogo tulilazimika kumuhamisha na kumficha mahali apate huduma kwa siri. Mimi niliporudi nyumbani Peris sikumwona nilijaribu kupiga simu yake ikawa haipatikani. Nikaamua kulala halafu asubuhi niende kufuatilia taarifa zake kule kituoni anakofanyia kazi. Usiku ukapita asubuhi nikaamka na kuanza kuelekea kituoni. Nilipofika nilimkuta mkuu mpya nikamweleza shida yangu naye akaniambia kuwa Peris hajaonekana kazini kwa mda wa siku tatu mfululizo. Tuliongea mambo mengi sana mpaka nikamweleza kua mimi ndo nilikua mkuu pale ila nilisimamishwa bila sababu za kueleweka.
Alikua mwelewa sana hali iliyonifanya nijisikie furaha. Alinisikiliza kwa makini na kisha akasema kama ni majambazi ndiyo napambana nao yeye atanipa ushirikiano wa kutosha. Nipambane nikiwa kama nimesimamishwa lakini kama kuna msaada wa kijeshi nitauhitaji nimwabie. Tulikubaliana mambo mengi hata kusema atafuatilia nirudi kazini. Nilifurahi sana nikaamua kuondoka na kwenda hospitalini. Nilifika nikamwona yule kijana akiwa anaendelea vizuri sana. Sikutaka kumuhoji maswali mengi mda ule niliamua kuongelea mambo mengine tuu. Nilimsaidia kunywa chai kisha tukawa tunapiga stori hapa na pale. Mda ukasogea siku zikaenda huku nikiwa sijui Peris alipo tangu alipotoweka siku ile hospitalini.
Ulifika wakati tukaruhusiwa na yule kijana. Kwakuwa kijana alikua chini yangu ilibidi niende naye nyumbani kwangu. Tulipofika ilinibidi niwe naye kila sehemu niendapo ili kuhakikisha usalama wake. Nilianza kumfanyisha mazoezi na kumpa vyakula vizuri ili ajenge afya. Alirudi kwenye hali ya kawaida hakika alikua jembe sasa. Kuna siku moja tulipanga kwenda kumtembelea yule mku mpya wa kituo. Nilimwita mdogo wangu akaniita kaka. Alifurahia uwepo wangu na mimi pia. Baada ya kufika kwa yule mkuu. Mimi ndiye nilikua wa kwanza kushuka kwenye gari. Wakati nashuka kuna pikipiki niliona ikija kasi pale nyumbani kwa mkuu. Nilibaki nimeduwaa naangalia ni nini kitajiri.
Yule mtu alifika na kupaki pikipiki kisha akashuka na element hakuvua. Hivyo sikumtambua. Hakusalimia na akaingia kwa kasi ndami. Kwa kua alivaa suruali nilijua kua ni mwanamke kwa umbo na mwendo wake. Baada ya kama sekunde 30 alitoka kwa kasi na kuwasha pikipiki na kutoweka. Hali ile ilinitia mashaka nikaamua kuingia ndani ndipo nikakuta mke wa mkuu kapigwa risasi. Nilijaribu kumtafuta mkuu hakua anapokea simu nikaamua kumkimbiza hospitali mama yule. Mkuu alipokuja alifika na kukuta mke wake yuko chini ya uangalizi wa madaktari. Basi alinishukuru sana. Wakati tunarudi nyumbani njiani nikamkumbusha yule kijana juu ya zile picha. Akambia ule mkanda aliuficha Sinza makaburini kwenye kaburi fulani pale.
Usiku ulikua umefika tukaamua tulale kwanza kisha asubuhi ndo twende tukachukue. Asubuhi ilipofika safari ya kwenda si nza makaburini ilianza. Tulipofika makuburini yule kijana akaanza kutafuta kile kitu eneo lile na mimi kwa mbaali nikaona kule getini kuna mtu anapiga honi sana akiashiria nimepaki gari njiani. Nikamwambia yule kijana Oscar ngoja nikatoe gari njiani ukiukuta njoo nao. Akajibu sawa brother.
Nilipofika mikahamisga gari jamaa akapita. Nilikaa kusubiri kuona kama Oscar atakuja lakini hakua anakuja nikaamua kumfuata. Lakini wakati naenda nikawaona kama vile wako wawili wakibishana yule wa pili alikua ni mwanamke. Nikajiuliza ni nani yule? Na wanabishana nimi? Nikaamua kuongeza mwendo lakini kadri nilivyozidi kusogea nilikua naisikia ile sauti kama naifahamu hivi. Nilikaza mwendo na kuwakaribia Mungu wangu sikuamini ninachokiona mbele yangu alikua ni Peris akiwa amejifunga ushungi fulani kichwani.
Alipoona nasogea kwa kasi akatoka mbio. Tukaanza kukimbizana mle makaburini. Chakushangaza ni kua Oscar hakua ananisaidia. Nilitafuta bastola nikakumbuka nimeiacha kwenye gari hivyo silaha pekee ni kumkamata na kumtia ngumi za uhakika. Alikimbia kwa kasi sana mpaka getini kisha kuna gari akaingia na wakatoweka. Nikarudi kumfuata Oscar huku makaburini. Nilipofika nikaanza kwa kumfokea oya dogo mambo gani sasa unamwona adui halafu hata hunisaidii kumkimbiza!
Ndipo akainua uso huku akilia. Nikamwuliza tatizo nini akanionyesha mguu. Kulikua na kisindano kidogo alikichoma Peris kilifanya ule mguu kuvimba sana ndani ya mda mfupi. Nilikichomoa kile kisindano kwa nguvu kisha nikamuuliza vipi? Akajibu bro nahisi maumivu makali sana siwezi hata kusimama nisaidie bro. Nikambeba mpaka kwenye gari ili nimuwahishe hospitali. Alikua analia sana Oscar lakini kabla ya kuondoka ilinibidi nimwulize kilichotupeleka kama kimefanyika. Eeenhe vipi dogo uwo mkanda wa picha umeupata? Au nao umeporwa na mwanaharamu yule? Kama umeporwa nimekwisha! Uko wapi? Nilimwuliza maswali mfululizo kisha nikatulia kidogo! Nikasema nijibu basi. Ndipo kwa sauti ya kulia lia akajibu kuwa__________________________
EmoticonEmoticon