MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA
Sim no, 0755683295/Watsap, Email@yusuphngahala@gmail.com, Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala, Instagram@mwalim_yuu.
SEHEMU YA 23.
Tulipoishia Naishi kwa mashaka je raia wa kawaida waishije sasa? Nikiwa najiuliza hayo maswali mara nikaona damu inatiririka chini ya mlango wangu ikitokea nje kuingia ndani......... Endelea.......Woga ukanijaa, nilikua najiulaza damu inatokea wapi? Nilihisi harufu ya umauti inanukia mbele yangu. Nikasogea pembeni labda nitaona mlango unavunjwa lakini hali ilikua tofauti. Kimya kilitanda na woga ukazidi kuitawala roho yangu. Nikaamua kujitoa fahamu na kufungua mlango ili kama kuna mtu au watu nikabiliane nao. Nikasogea mbele kidogo nikashika mlango na kisha nikauvuta.
Chaajabu sikuona kitu chochote zaidi ya kuona hali ya hewa tulivu. Nikatoka na kukagua kagua nje kabda nitaona chochote lamini hali haikua hivyo. Mapigo ya moyo yalikua yanaenda kasi sana mate mdomoni yalinikauka. Nikawa naingia ndani ili nifikirie nifanye nini? Mara nikasikia kwa mbali kama kuna watu wanaagana nje. Nilipofanya jitihada za kuchungulia nilimwona mke wangu Peris akiagana na mtu ambae hata sikumjua.
Alipofika na kuniona katika hali ile akaniuliza vipi Yuu mbona uko juu juu? Na mbona mlangoni kuna damu? Kuna nini? Niliona ananichanganya tuu ukizingatia na yeye nilishajua kua si mtu mzuri. Nilimkalia kimya bila kumjibu chochote mpaka akashangaa. Basi usiku ule ukapita salama na siku zikasonga huku mimi nikizidi kujituma nikamilishe kesi yangu ili nirudi kazini. Cha ajabu ni kua katika kila hatua nilikua nagundua usaliti mkubwa sana ndani ya jeshi la polisi. Hali ile ilikua ikinitisha sana. Kuna siku nilitoka nyumbani na kwenda mahali fulani wakati narudi nyumbani nilihisi ndani mwangu kuna watu wasio wema.
Nilishuka taratibu kwenye gari yangu. Taratibu nikajihami na kuanza kuelekea mle ndani kisha nikasukuma mlango kwa nguvu na luanza kumimina risari kwa mfululizo. Baada kama ya dakika moja hivi nilitulia na kuona kuna watu wawili wameanguka chini. Walikua wamevalia vinyago vya kuficha nyuso zao. Baada ya kukagua nyumba na kuhakikisha hakuna mwingine nikawafunua vlzile sura zao na kujikuta simtambui hata mmoja.
Nikatoa taarifa polisi wakaja na kuchukua miili ile. Kuna siku nikapigiwa simu na mtu nisiyemjua akadai anahitaji kuonana na mimi. Ilikua ngumu kidogo kumwelewa lakini baadae ikanibidi ndipo baada ya kumwona alikua ni kijana mchafu kiasi na mwenye kuchoka kimaisha alikua ananuka jasho na alivalia yeboyebo zilizoisha upande. Nikamwuliza enhee shida yako ndipo akasema mimi ndiye nilikupiga picha! Nikamwuliza sasa unatakaje? Akajibu ni kwamba sikufanya kwa matakwa yangu bali nilitumwa na niliahidiwa pesa lakini mwisho wa siku hata pesa sikupata na kamera walichukua na bado wananitishia kifo.
Sababu ya kunitishia kifo ni kwasababu baada ya kuhisi ubabe wao nilibadilisha mkanda ndani ya kamera. Niliweka wenye picha zisizo zako hapo ndipo vita ikaanza. Nikamwuliza na huo mkanda uko wapi basi wakati anataka kusena ghafla alioigwa risari na mtu asiyejulikana. Nilitoka pale na kumfuatilia yule aliyerusha risasi naye akawa anakimbia kwa kasi. Nikaamua kurudi ili nimkimbize hospitali yule kijana. Kwani sehemu aliyopigwa ilikua na uwezekano wa kupona akiwahishwa. Niliita teksi mara moja nikamuwahisha hospitalini. Tulipofika alihudumiwa haraka sana. Hii ilitokana na mimi kujulikana pale hospitalini na pia ucheshi wangu.
Baada ya mda nikaambiwa bado yu hai ila atachelewa sana kuzinduka. Niliwashukuru sana madaktari kwa jtihada zao. Kisha nikaondoka ili nifike nyumbani mara moja. Baada ya kufanya kilichonipeleka nyumbani nikatoka na kuanza kuelekea hospitalini. Chaajabu ni kua Peris alinipigia simu na kuuliza Yuu uko wapi nikamjibu nyumbani. Akasema unatoka saa ngapi nikamjibu hapana mimi nipo kwani vipi? Akajibu hapana nauliz a tuu. Kisha akakata simu. Alionekana kama mwenye wasisiwasi fulani. Nilijua lazima kuna namna kwani tayari Peris nilikua simwamini tena! Na kilichokua kinanifanya nizidi kuishi naye nilikua natafuta ushahidi wa kumtia mbaroni.
Alipokata simu sikutaka kujishuhulisha naye mi nikazidi kusonga mbele na mambo yangu. Kuna mahali nilipita nile kidogo kisha nichukue chakula kwaajili ya mgonjwa wangu. Wakati nimekaa pale kuna mtu alikua akiniangalia sana. Kwa kipindi hiki nilikua mbabe sana sikujua ni hasira au ni nini kilinifanya kua vile. Nikamfuata na kumzibua bonge moja la kofi kisha nikamwuliza mbona unaniangalia sana? Mwingine akadakia kwani kukuangalia ni kosa? Nikageuka kumfuata naye aliponiona akatoka nduki. Nilirudi ili nimalizane na yule niliyempiga naye hakuwepo tena.
Nikarudi na kuchukua chakula changu kisha safari ya hospitalini ikaendelea. Nikiwa njianinilipokea ujumbe mfupi wa maneno. Ambao namba ya mtumaji ilioekana jina Zabroni kisha ukasomeka hivi AMA KWELI UMEVURUGWA SIKU HIZI Nilijua tuu kua wale watu pale hotelini si wema. Nikarudisha simu kisha nikafika hospitalini. Nilishuka na kuchukua chakula kuelekea alikolazwa yule kijana. Taratibu nikalikaribia wodi. Lakini wakati nafikia wodi nilimwona nesi akimaliza kumchoma sindano kiheshima sikupaswa kuingia. Nikasimama nje mara nesi akawa natoka. Tukakutana mlangoni. Haa hakuwa nesi niliyemtarajia bali alikua ni Peris amevalia mavazi ya manesi. Peris mke wangu alishtuka kiasi kisha_______________,_________
EmoticonEmoticon