Meya
Mteule wa jiji la Mbeya Diwani wa Kata ya Nzovwe(CHADEMA) Ndugu David
Mwasilindi ambaye aliibuka kidedea kwa kupata kura 34 dhidi ya Mpinzani
wake wa CCM aliyepata kura 14 katika uchaguzi uliofanyika Desemba 10
katika ukumbi wa Mkapa jijini humo.
|
Katibu
Tawala Wilaya ya Mbeya Ndugu Quip Mbeyela ambaye ndiye aliyekuwa
Mwenyekiti katika Kikao cha Baraza la Madiwani ambacho kiliketi kufanya
uchaguzi wa kumpata Meya wa jiji hilo pamoja na Naibu Meya katika
Halmashauri ya jiji la Mbeya .
|
Kaimu
Mkurugenzi Halmashauri ya jiji la Mbeya Dkt Samuel Lazaro akizungumza
katika kikao cha Baraza la Madiwani ambalo liliketi kwa ajili ya
kumchagua Meya pamoja na Naibu Meya katika Ukumbi wa Mkapa jijini humo.
|
Kaimu
Mkurugenzi Halmashauri ya Jiji la Mbeya Dkt Samuel Lazaro akiteta jambo
na Meya Mteule wa jiji la Mbeya Mh.David Mwasilindi katika kikao cha
Baraza la Madiwani Halmashauri ya jiji hilo.
|
Wajumbe wa baraza la Madiwani Halmashauri ya jiji la Mbeya wakifuatilia kwa umakini majadiliano katika mkutano huo.
|
Baadhi
ya watumishi wa jiji la Mbeya wakiteta jambo katika mkutano huo wa
baraza la Madiwani la Halmashauri ya jiji la Mbeya ambalo liliketi na
kumchagua Meya na Naibu wa jiji hilo ambaye ni David Mwasilindi (CDM)
baada ya kupata kura 34 dhidi ya mpinzani wake wa CCM aliyepata kura 14.
|
Diwani akizungumza katika baraza hilo.
|
Madiwani
wakiimba wimbo wa taifa baada ya kukamiliza zoezi la uchaguzi katika
baraza hilo la Madiwani halmashauri ya jiji la Mbeya .
|
Baadhi
ya wananchi na wafuasi wa vyama mbalimbali jijini mbeya wakifuatilia
kwa umakini uchaguzi wa kumpata Meya wa jiji la Mbeya na Naibu Meya
wakiwa nje ya ukumbi wa Mkapa jijini humo .
|
Tukifuatilia Mkutano .
|
Na EmanuelMadafa,Mbeya
Hatimaye
Halmashauri ya jiji la Mbeya limepata Meya wake mara baada ya kufanyika
kwa uchaguzi wa kugombea nafasi ya Meya na Naibu Meya watakaoongoza
halmashauri ya jiji la Mbeya katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Meya
huyo mpya wa jiji la mbeya ametokana na Chama cha Chadema Mch David
Ponela Mwashilindi kutoka kata ya Nzovwe pamoja na Naibu wake Mch
David Nelson Ngogo kutoka kata ya Nsalaga ambao wote wametokana na
chama hicho.
Katika
uchaguzi huo uliofanyika Desemba 10 kwenye ukumbi wa Mkapa na
kusimamiwa na Katibu tawala wa wilaya ya Mbeya Quip Mbeyela,alimtangaza
mshindi wa Umeya kuwa ni Mwashilindi aliyepata kura 34 akimshinda
mgombea wa nafasi hiyo kutoka CCM,Kefas Mwasote Changani aliyeambulia
kura 14.
Kwa
upande wa nafasi ya Naibu Mbeya mshindi wa kura nyingi aliyetangazwa ni
Mch Ngogo(Chadema) aliyeipata kura 34 dhidi ya mgombea wa CCM katika
kinyang’anyiro hicho,Modest Pantaleo Shiyo aliyeambulia kura 14 na hivyo
kukifanya chama cha Chadema kuongoza halmashauri ya jiji hilo.
Mara
baada ya kutangaza matokeo hayo yaliyowashirikisha madiwani wa Chadema
34 dhidi ya wale wa CCM 14,msimamizi wa uchaguzi huo,Mbeyela alisema
kuwa vyama vyote vilivyoshiriki kwenye mchakato huo sasa umekwisha na
wanachotakiwa kukifanya madiwani wote ni kuchapa kazi kwa nguvu ili
kusukuma kwa kasi maendeleo ya jiji hilo.
Akizugumza
mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa nafasi ya Naibu Meya,Ngogo
alisema kuwa atahakikisha kuwa anaheshimu haki na uhuru wa kila diwani
katika kushauri na kutoa maoni bila kujali itikadi ya vyama vyao kwa
kuwa kazi kubwa iliyo mbele yao ni kuwatumikia wananchi wote.
Mstahiki
Meya wa jiji hilo kutoka Chadema,Mwashilindi akiwashukuru madiwani wote
kwa kura nyingi alizopigiwa,alisema kuwa atahakikisha kuwa
anashirikiana na madiwani wote na kuhakikisha kuwa kata zote za jiji
hilo zinapiga hatua kubwa na huo ndio mtazamo wake.
Kaimu
Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji hilo,Dk Samwel Lazaro alisema kuwa
atahakikisha watendaji wa halmashauri hiyo wanatoa ushirikiano wa
kutosha kwa madiwani wote pale wanapohitaji ufafanuzi wa kitaalamu ili
kila jambo wanalotaka kulifahamu wapate kwa wakati.
Mwisho.
(Jamiimojablog-Mbeya
EmoticonEmoticon