TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS
RELEASE” TAREHE 12.05.2015.
·
MTU MMOJA AFARIKI DUNIA NA WENGINE KUJERUHIWA
KATIKA AJALI YA BARABARANI MKOANI MBEYA.
·
JESHI LA POLISI MKOA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU
WAWILI WAKIWA NA POMBE MOSHI UJAZO WA LITA 51.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE, JINSI
YA KIUME, UMRI KATI YA MIAKA 35 - 40 ALIFARIKI DUNIA BAADA YA GARI WALIOKUWA
WAKISAFIRIA YENYE NAMBA ZA USAJILI T.197
AGV AINA YA TOYOTA COASTER ILIYOKUWA IKITOKEA MBEYA KUELEKEA KYELA
IKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE JUSTINE
DANIEL (45) MKAZI WA TUKUYU KUGONGA NYUMBA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.886 AHY AINA YA M/FUSO LORI
LILILOKUWA LIMEEGESHWA BAADA YA KUHARIBIKA.
AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 11.05.2015 MAJIRA YA SAA
19:20 JIONI HUKO KATIKA KIJIJI CHA GARIJEMBE, KATA YA GARIJEMBE, TARAFA YA
ISANGATI, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA
MBEYA/TUKUYU.
AIDHA KATIKA AJALI HIYO, WATU WATATU WALIJERUHIWA
AMBAO NI 1. DEREVA WA TOYOTA COASTER
JUSTINE DANIEL (45) 2. LUGANO
MWAKIPESILE (47) MKAZI WA UYOLE NA 3.
MTOTO YESE EMANUEL MWENYE UMRI WA MIEZI MINNE. MAJERUHI WAMELAZWA HOSPITALI
YA RUFAA MBEYA. CHANZO CHA AJALI
KINACHUNGUZWA. DEREVA AMEKAMATWA.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI NYIGESA R. WANKYO
ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI
PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI
ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
TAARIFA ZA MISAKO:
KATIKA MSAKO WA KWANZA, JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA
MKAZI WA KYELA-KATI AITWAYE MWALIFUKO
MWASAMBOGO (38) AKIWA NA POMBE
MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 49.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 11.05.2015 MAJIRA YA SAA
15:30 JIONI HUKO KATIKA ENEO LA KYELA-KATI, KATA YA KYELA-KATI, TARAFA YA
UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA.
KATIKA MSAKO WA PILI, JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA KAJIGILI
MWAKANOSYA (20) MKAZI WA ITUHA
JIJINI MBEYA AKIWA NA POMBE MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 2.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 11.05.2015 MAJIRA YA SAA
13:00 MCHANA BAADA YA KUFANYIKA MSAKO HUKO KATIKA ENEO LA ITEZI, KATA YA
ITEZI, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA
MAHAKAMANI WATUHUMIWA ZINAENDELEA.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI NYIGESA R. WANKYO
ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA
SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Imesainiwa
na:
[NYIGESA R.
WANKYO – ACP]
KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon