SIMULIZI YA KUSUSIMUA-NANI KACHUKUA SURA YANGU?SEHEMU YA 26

Displaying sehem ya 26.jpg

MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.

Sim no,0755683295/Watsap, Email@yusuphngahala@gmail.com, Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala, Instagram @mwalim_yuu.

=SEHEMU YA 26:
Tulipoishia, Alipoongea akisema tulia hapohapo ile sauti ilikua ya Peris kabsaa. Hali ile ilinifanya nitake kujua zaidi nikawa nazidi kumsogelea. Mara mlio wa risasi ukasikika Paaaaaaa!!!!!!!!_______

Endelea_____ Nilihamaki na kushangaa nani kapiga risasi. Wakati nashangaa mlio ulipotokea ile hali ilimpa mwanya Peris wa kutoka. Niliposhtuka alikua tayari kapotelea nje. Nikatoka na kuangalia hapakuwa na mtu nikarudi ndani na kumwona Oscar akiteseka. Nilimwinua na kumwangalia nikampa huduma ya kwanza kisha nikaanza kuangalia kama kuna chochote mle ndani. Nikagundua kuwa vile vitu nilivyovikusanya siku ile kwenye jumba la majambazi. Na pia zile sura zabandia nilizozitoa nyumbani kwa Peris zilikua zimechukuliwa.

Nililaumu sana kile kitendo kwani tayari juhudi zangu za kuwakamata zilirudishwa nyuma. Ushahidi ulikua ukipunguzwa. Nilijilaumu sana. Usiku ule sikulala kabisa asubuhi saa 11 alfajiri niliwahi kituoni nikafika na kuwaamuru vijana waliolala shifti ya usiku kuezeka kituo.ilipofika saa 12 nilichukua kikosi kingeni cha askari 15 hodari ambao niliwaamini sana. Tukatoka na kwenda kuvamia lile jumba la majambazi kule nilikoenda mara ya kwanza.

Hakuna hata askari mmoja niliyemjuza kua tunaenda wapi, niliwaamuru simu zao waache kituoni. Hali ile ilikua msaada kwani hata waliozoea kuvujisha siri za kituo ilikula kwao. Tulifika pale kisha nikaamrisha kila kilichopo mbele ni halali yako. Ni mwiko kurudi nyuma. Kwa kulitetea taifa letu na kulipigania kama tulivokula kiapo shambulia hapa. Mashambulizi yasiyo na kikomo yakaanza.

Tulisonga mbele huku risasi zikimiminwa bila kukoma. Mara wakati tunaingia ndani tukasikia mashambulizi kutokea ndani. Hii iliashiria wapo tulizidi kusonga huku tukijibizana risasi kwa kasi na majambazi mle ndani. Tukiwa ndani tuligawana kimakundi wengine wakasonga upande wa pili. Baada kama ya dakika 20 hivi hali ikatulia mle ndani. Tukawa tunakusanya majeruhi na maiti pale za washukiwa wa ujambazi.

Mimi nilihisi lazima kuna wengine wamejificha nikaanza kuingia chumba hadi chuma. Nilifanikiwa kukamata majambazi watatu. Chaajabu ni kua katika idadi ya watu 18 tuliowakamata idadi ya watu 11 walikua ni askari wanaolitumikia jeshi la polisi na tunawafahamu kabisaa. Hali ile ilinishitua mbaya zaidi wa kituoni kwangu walikuwa 5 bahati mbaya 4 walikua wameshapoteza maisha. Nikaamrisha kufanya upekuzi mle ndani na askari kadhaa wakafanya kazi hiyo. Baada ya mda nikaomba msaada wa magari kutoka kituoni.

Baada ya magari kufika walipakiwa mateka wote pamoja na maiti. Kisha tukaenda nao kituoni kwa mahojiano. Huku nyuma magari mengine yalipakia vitu vyote vilivyopatikana mle ndani. Ikiwa ni pamoja na mabomu, silaha mbalimbali, sare za jeshi la wananchi JWTZ na madawa ya kulevya. Sumu kali za maangamizi vinasa sauti na vingine vya kihalifu vingi sana.Tulifika kituoni na kuwashusha wachache wale wazima kabisa. Majeruhi walipelekwa hospitali na maiti walipelekwa mochwari.

Wale wazima sikutaka hata kupoteza mda. Niliwaingiza chumba cha mahojiano. Huko nikaanza kuwahoji mmoja baada ya mwingine. Walikua wanasumbu kiasi. Nikaamua kutumia nguvu sasa. Wengine nikawafunga na pingu pembeni nikaanza na mmoja. Nikamwuliza maswali hakua ananijibu nikamzibua ngumi ya akili usoni. Kisha nikamwangalia. Majambazi wanadharau aisee. Badala y a kunijibu akanitemea mate usoni hapo ndipo nikasema leo ndiyo leo.

Nilijifuta mate kisha nikachukua shoti za umeme nikawa nampiga nazo. Bado hakusema nani yuko nyuma yao. Nilimuhoji sana hakusema ikabidi nichukue "prize" nianze kuminya korodani bado hakusema alikua akilia tuu bila machozi. Nikaanza kumvunja vidole mpaka vidole vyote vikaisha hakika alikula kiapo yule jambazi. Nilihamia kwenye meno na kuanza kung'oa moja baada ya jingine bado hakusema. Zaidi alisema tuu kua yeye alikua ni mwanajeshi na alipofukuzwa ndipo alijiunga na kundi lile. Nilipomwuliza anayewatuma kuua na kufanya uhalifu ni nani hapo ndipo alikataa kusema.

Nilifanya kila juhudi nilitoa meno zaidi ya nane lakini wapi. Nilifanya kila mbinu lakini ilishindikana. Yaani alikua akilinda kiapo chake cha ujambazi kuliko kawaida. Nikaamua akae pembeni niendelee na wa pili hapo ndipo nikapigiwa simu na mkuu na kuambiwa kuna ofisi ya ubalozi fulani imezingirwa hivyo niandae kikosi mara moja. Nilifurahi kwa kuwa imani ya viongozi wakubwa imerudi tena kwangu. Nilipomwuliza idadi ya majambazi akanambia inahitajika nguvu kubwa.

Ndipo nikaamua kuwarudisha wale majambazi mahabusu. Kisha kituoni nikabakiza askari watatu kwa ulinzi. Wengine tukatoka hadi ubalozini na tulipofika tulikuta majambazi tayari wamwtoweka na hawakufanya tukio lolote pale. Baada ya kuhakikisha usalama wa pale na kujiridhisha nikabakiza askari kadhaa kwa ulinzi zaidi kisha nikageuza gari. Wakati nikiwa njiani simu yangu ikaita nikapokea simu na kusikia sauti ya Zabroni ikisema sasa umelianzisha.

Sikujali nikakata simu na kuendelea na safari yangu. Kisha nikafika kituoni na wakati nashuka nilikuta hali iko tofauti . Askari walikua wameuawa. Nilipoingia mahabusu sikuona kitu nikajua pale tulichezewa na Zabroni ili kuwaokoa nduguze. Nikakumbuka wengine wako hospitali. Nikawasha gari hadi hispitali na nikamfuata nesi wa zamu nikamwuliza vipi wagonjwa wangu.Ndipo akanijibu afande we si umekuja hapa ukaamuru wahamishwe? Nilishtuka kisha nikamwambia mimi sijaja hapa. Akazidi kusema afande ni wewe na uliamuru kufanya hivo mara moja. Mbona unatushangaza umerudu kuuliza tena. Nilijua tuu huenda Zabroni kapita. Nikiwa nimeduwaa mara simu yangu ikaita kuangalia nani anapiga alikua ni Peris nikapokea kisha nikasikia_____________________
__________________________________________________________________________________________________________________________________Kutana na mimi swhemu ya 27 ujue nini kilifuata au siyo? Nawapenda wote na nafurahi kwa sapoti yanu. Tuko pamoja sana kwa lolote mawasiliano yapo hapo juu.👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆🙏
Previous
Next Post »