TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 28.04.2015.







Ø  WATU WATATU WASIOFAHAMIKA WANYANG’ANYA GARI [W] MBALIZI  NA KISHA KUSABABISHA  AJALI YA  WATU WAWILI KUFARIKI WILAYA YA MBEYA.


Ø  MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI ILIYOHUSISHA GARI NA PIKIPIKI WILAYA YA MBALIZI.



Ø  WATU WANNE WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA MAKOSA YA KUPATIKATIKANA NA POMBE YA MOSHI WILAYA YA MBEYA NA CHUNYA.



Ø  JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA WAHAMIAJI HARAMU 13 RAIA WA NCHINI BURUNDI WILAYA YA ILEJE.


TUKIO LA KWANZA.

WATU WATATU WASIOFAHAMIKA WALINYANG’ANYA GARI T.640 CDE AINA YA TOYOTA IPSUM MALI YA NICHOLAUS MASHAKA [26], MKAZI WA MBALIZI II, LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA TAXI DRIVER FRANK STAFORD [23], MKAZI WA NDOLA-MBALIZI.

TUKIO HILO LILITOKEA TAREHE  27.04.2015  SAA 21:00HRS  USIKU  HUKO KATIKA ENEO LA ST MARY MBALIZI, KATA YA SONGWE,TARAFA YA USONGWE BAADA YA WATU HAO KUMKODI DEREVA ILI AWAPELEKE KIJIJI CHA IWALA KUCHUKUA MGONJWA NA NJIANI KUMFUNGA KAMBA, KUMTUPA VICHAKANI KISHA KUONDOKA NA GARI HILO. MAJIRA YA SAA 23:30HRS WATU HAO WAKIWA NA GARI HILO ENEO LA UYOLE WAKIWA KATIKA MWENDO KASI WALIWAGONGA WANAWAKE WATEMBEA KWA MIGUU WAWILI 1. TELEZA JACKSON [38] NA 2. SNARA HENRY [36], WAKAZI WA UYOLE NA KUSABABISHA VIFO VYAO. BAADA YA AJALI HIYO WATU HAO WALIKIMBIA NA KULITELEKEZA GARI ENEO HILO.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WAENDESHAJI WA MAGARI YA BIASHARA AMBAYO HAYAJASAJILIWA KUFANYA BIASHARA  (TAXI  BUBU )NA PIKIPIKI @ BODABODA WAKASAJILI ILI KUWEZA KUBAINI HATA IKIIBIWA NA VILEVILE  KUTOWEKA TINTED ILI KUWEKA TAHADHALI PINDI WANAPOSAFIRISHA ABIRIA WASIOWAFAHAMU HASA USIKU. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI WALIPO WATU HAO AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE MARA MOJA DHIDI YAO.

TUKIO LA PILI:

MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI ILIYOHUSISHA GARI NA PIKIPIKI WILAYA YA MBALIZI.

 MWENDESHA  PIKIPIKI T. 990 AAJ AINA YA SKY MARK AITWAE ANTHONY MWESENGA [28], MKAZI WA MBALIZI ALIFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI T.296 BGE AINA YA M/CANTER LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA NURU NICKSON [34],MKAZI WA MBALIZI.

TUKIO HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE 27.04.2015 MAJIRA YA SAA11:30  JIONI HUKO KATIKA KIJIJI CHA KESALIA, KATA YA UMALILA,TARAFA YA ISANGATI WILAYA YA KIPOLISI MBALIZI, MKOA WA MBEYA,  BARABARA YA UMALILA/MBALIZI.  CHANZO CHA AJLI HIYO BADO KINACHUNGUZWA. MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA NA WATEMBEA KWA MIGUU KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA

KATIKA MISAKO

WATU WATANO WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA MAKOSA YA KUPATIKATIKANA NA POMBE YA MOSHI WILAYA YA MBEYA NA CHUNYA.


TUKIO LA KWANZA:
 MTU MMOJA CHRISTINA MBANGA [47], MKAZI WA MAKUNGULU, ALIKAMATWA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 5.

TUKIO HILO LILITOKEA TAREHE 27.03.2015 MAJIRA YA SAA 12:15HRS HUKO KATIKA EENO LA JUAKALI, KATA YA MAANGA, TARAFA YA IYUNGA JIJINI MBEYA. TARATIBU ZINAFANYWA ILI MTUHUMIWA AFIKISHWE MAHAKAMANI.

TUKIO LA PILI

AIDHA KATIKA TUKIO LA PILI.  WATU WATATU  IKUPA ALLY  {26},MKAZI WA MAKUNGULU,   EMANUEL  RAPHAEL [29],MKAZI WA MWANJELWA NA GEOFREY JEREMIA [31],MKAZI WA ISYESYE   WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI BAADA YA KUKAMATWA WAKIWA NA POMBE YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 5.

TUKIO HILO LILITOKEA TAREHE 27.04.2015 MAJIRA YA SAA 13:10HRS HUKO KATIKA ENEO LA JUAKALI, KATA YA MAANGA,TARAFA YA IYUNGA JIJINI MBEYA.TARATIBU ZINAFANYWA ILI WATUHUMIWA WAFIKISHWE MAHAKAMANI.

TUKIO LA TATU:

MTU MMOJA YELA MWASILE [45], MKAZI  WA UPENDO, ALIKAMATWA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI UJAZO WA LITA 5.

TUKIO HILO LILITOKEA TAREHE 27.04.2015 MAJIRA YA SAA 19:00HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MAJENGO, KIJIJI NA KATA YA  TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUHNYA MKOANI MBEYA.

TUKIO LA NNE:

JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA WAHAMIAJI HARAMU 13 RAIA WA NCHINI BURUNDI WILAYA YA ILEJE.

WAHAMIAJI HARAMU  13 RAIA NA WAKAZI WA NCHINI BURUNDI WAMEKAMATWA KATIKA KIJIJI CHA ISONGOLE,KATA YA ISONGOLE,TARAFA YA BULAMBYA.

TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE  27.04.2015 SAA 21:30HRS KIJIJINI HAPO JIRANI NA MPAKA WA TANZANIA NA MALAWI WAKIWA WAMETOKEA NCHINI MALAWI.

WAHAMIAJI HARAMU HAO NI 1. RUTON JOSEPH [71], 2. KWINZEYA JEREMIA [27] 3. FREDY SHUTINAMAGAGARA [29] 4. ENDAKUMANA LEWANCE [24] 5. NIYONZURU ALBER [30] 6. ATANGAMANA ELISA [25] 7. NIYOKUSENGA SHARIOT [ 5], 8. HAFASHIMANA ADELINE [10], 9. NIMPAYE FAINES [7] 10.NIYONZIMA CHANINE [27] 11. MOGISHA FRANK [1] 12. SABUSHIMIKE ANISETI [33] NA 13. SABUSHI MIKEME [12]. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAKABIDHIWE IDARA YA UHAMIAJI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA JUU YA MTU/WATU WANAOWATILIA SHAKA IKIWEMO RAIA WA KIGENI ILI HATUA/UCHUNGUZI DHIDI YAO UFANYIKE.


Imesainiwa na
[AHMED  Z. MSANGI – SACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Previous
Next Post »