TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI [PRESS RELEASE] TAREHE 26.04.2015.







MNAMO TAREHE 24.04.2015 MAJIRA YA SAA 09:30 ASUBUHI HUKO MAENEO YA MTAA WA SOGEA KATIKA MJI MDOGO WA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA, VIJANA WAWILI WALIOTAMBULIKA KWA MAJINA YA 1. MATHEW ANGANILE MWAFONGO @ RASI (27) MKAZI WA TUNDUMA NA MWENZAKE AITWAYE SALEHE TABULEI SICHALWE (22) MKAZI WA MAJENGO TUNDUMA WALIKAMATWA NA POLISI BAADA YA WANANCHI WA ENEO HILO KUWATILIA MASHAKA KUWA NI WAHALIFU, HII NI KUTOKANA NA MVAO WAO AMBAO ULIKUWA UMEFICHA SURA ZAO.

VIJANA HAO WALIKUWA WAKITUMIA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.855 CDQ AINA YA T-BETTER NA WALIKUWA NA BEGI MOJA AMBALO MMOJA WA VIJANA HAO ALIKUWA AMELIVAA MGONGONI.

POLISI WALIPOWAPEKUA KATIKA BEGI HILO WALIKUTA VISU VIWILI, MANATI MBILI, MAWE AROBAINI YA KURUSHWA KWA MANATI NA NATI NNE ZA KURUSHWA KWA MANATI, KOFIA MBILI ZA JESHI, BUTI JOZI MBILI, MIWANI MIKUBWA INAYOTUMIWA NA POLISI KATIKA MISAFARA, SHEEGUARD JOZI NNE (VIFAA MAALUM VYA KUVAA KWENYE MAGOTI NA VIWIKO VYA MIKONO), MAKOTI MAWILI MAREFU, VIFAA VYA KUFANYIA MAZOEZI YA “PUSH UP” NA KAMBA YA KUFANYIA MAZOEZI YA KURUKA.

AIDHA KATIKA BEGI HILO KULIKUTWA PIA T-SHIRT MOJA YA CHADEMA, BENDERA MBILI NDOGO ZA CHADEMA, KITAMBAA/KILEMBA KIMOJA NA BARUA TATU ZA KUWATAMBULISHA WATUHUMIWA KWENDA KUTOA MAFUNZO KWA RED BRIGADE HUKO MAENEO YA KATA YA CHITETE, MSANGANO NA KAMSAMBA  WILAYANI MOMBA.


KATIKA KUHOJIWA, WATUHUMIWA HAO WALIKIRI KUWA WANAENDA KUTOA MAFUNZO KWA VIJANA WA RED BRIGADE KATIKA KATA HIZO TAJWA HAPO JUU. KUTOKANA NA MATISHIO TULIYONAYO YA USALAMA NA VIASHIRIA VYA UVUNJIFU WA AMANI NA UTULIVU NCHINI, WATUHUMIWA HAO WALIFIKISHWA POLISI MKOA KWA MAHOJIANO ZAIDI NA BAADA YA UCHUNGUZI, JALADA LITAPELEKWA KWA MWANASHERIA WA SERIKALI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANAWASHUKURU WANANCHI KWA KUCHUKUA TAHADHARI ZA KIUSALAMA KWA KUTOA TAARIFA HARAKA. AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA HARAKA KATIKA VYOMBO VYA USALAMA PALE WANAPOTILIA MASHAKA MTU/WATU AU VITENDO VYA MTU/WATU AU KIKUNDI CHA WATU ILI HATUA STAHIKI ZICHUKULIWE HARAKA IWEZEKANAVYO.

Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Previous
Next Post »