MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.
Sim no,0755683295/Watsap, Email@yusuphngahala@gmail.com, Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala, Instagram @mwalim_yuu.
SEHEMU YA KUMI NA TANO.
Tulipoishia Akajibu sawa nikamwambia lakini kua makini akajibu sawa. Lakini wakati nataka kukata simu mara kwenye simu nikasikia sauti ya mke wangu okilia kwa kelele za woga. Aaaaaaa! ____Endelea.........Muu.. Mumee waangu wanashuka wanashukaaa. Mara simu ikakatika. Nikajaribu kupiga ikaita bila kupokelewa. Nikapiga tena haipatikani. Nikahisi kuna kitu kibaya kimemtokea Peris wangu. Nikaamua kuwataarifu polisi ya kua Mwita kauawa hivyo waje kufanya uchumguzi. Nikawasha gari yangu kuwahi nyumbani. nilikimbiza gari kama kichaa. Baada ya kufika barabara kuu nikakutana na foleni kubwa. Nililaumu sana serikali yangu kwa kushindwa kuona mbadala wa kutoa foleni ile. Nikawa niko kwenye foleni lakini natamani nitembee kwa mguu. Nilipokumbuka kua Peris ni mjamzito roho iliniuma zaidi kwani nilijua wanaweza wakamfanyia unyama. Mke wangu wa kwanza walimuua na mwanangu. Tazama natarajia mtoto wa pili bado wamekuja nyumbani haa! Mawazo yakanituma nipaki gari pembeni kisha nichukue bodaboda.
Nikapaki pembeni na kuchukua bodaboda hadi nyumbani. Baada ya kufika nilimlipa yule kija hela yake kisha nikatoa bastola yangu. Nikaanza kulikagua eneo lile la nyumba yangu kwa umakini. Niliangalia lile gari sikuliona nikaamua kuingia ndani. Baada ya kuingia sebuleni nilikuta hali shwari hapakua na mtu. Tv ilikua imewashwa na inaonyesha. Nikaingia chumbani kwangu na kuona pia kuko shwari. Nikaanza kuwaza Peris na Anthony wako wapi? Nilipiga simu ya mke wangu Peris ilikua haipatikani. Nikaanza kuingiliwa na wasisi na kudhani huenda wametekwa. Ikumbukwe Peris alikua ni mjamzito wa miezi minne sasa. Nikatoka nje na kuangaliaangalia lakini sikuona dalili yoyote.
Nikaingia chooni mara moja nikojoe kisha nijue cha kufanya. Wakati nafungua mlango wa chooni ghafla nikamkuta Peris amelala mle chooni. Moyo ulilipuka kwa woga sikujua kama kalala au kafa. Nikamsogelea na kuanza kumtingisha. Nilimtingisha huku nikimwita lakini alionekana kuzidiwa na usingizi. Nilimwamsha sana hatimaye akaamka. Mmmh! Yuu vipi? Aliniuliza kama asiyejua kua alikua kalala chooni. Nikamjibu vipi mbona umelala huku? Akajibu haaa!! kwani umerudi saangapi? Umekuja na mboga? Alikua akijibu vitu vya ajabu ambavyo mimi sikumwuliza. Akili yake ilikua haiko sawa bado.
Nikamvuta na mkono nikamtoa nje. Baada kama ya sekunde kadhaa. Akasema Anthony yuko wapi? Wamemchukua? Haa amechukumliwa. Hapo akili ilianza kurudi. Nikamwuliza kwani imekuaje akajibu kuna mtu aliyekua akifanana na mimi alikuja na kundi la watu wanne. Walimchoma sindano na kumwambia aingie chooni. Ndipo hakujua imekuaje hadi mimi nakuja kumkuta kalala mle. Aliongeza kua yule mtu huenda ndiye Zabroni Makweka aliyekua akitusumbua siku zote. Nilipojaribu kuuliza watoto wa pale mtaani wakasema Anthony mimi ndiye niliyemchukua.
Nilijua tuu atakua ni Zabroni. Bahati mbaya hata sikujua wameelekea wapi. Niliumia sana kukamatwa kwa Anthony roho yangu ilimpenda kama mwanangu wa kumzaa. Niliumia haswaa. Niliona kichwa kinakua kizito sana. Nilimpenda Anthony lakini ningefanya nini? Nilibaki kujililia tuu. Mke wangu Peris na mimba yake alikua kachanganyikiwa mpaka basi. Nilimhurumia sana. Nikawalaani sana akina Zabroni na kundi lake. Nikiwa na majonzi pale nalia nikapokea simu kutoka kwa afande mwenzangu Upendo. Akasema Yuu kuna uvamizi eneo la maili moja nje kidogo ya jiji la Dar es salaam. Mabasi kadhaa ya abiria yametekwa na njia zimefungwa. Tayari kuna vikosi kadhaa kule ila inahitajika nguvu zaidi. Nilikula kiapo kua tayari mda wowote jeshi likinihitaji. Ikabidi nianze safari ya kuondoka kuelekea kituoni.
Peris hakutaka niondoke alikua akilia sana. Lakini ilinilazimu. Nikamwelekeza mahali nimeacha gari ili akaifuate. N ilifika kituoni na kuandaa kikosi cha mashambulizi. Baada ya mda difenda mbili ziliondoka kituoni zikiwa zimesheheni maafande shupavu. Mimi mwenyewe nikiongoza msafara na pikipiki aina ya baja. Hakika tulijipanga. Barabarani tulipita huku tumewasha taa nyekundu, king'ora na bendera nyekundu zilifungwa kuashiria hatari.Baada ya kufika eneo la tukio tulisikia majibizano ya risasi baina ya polisi waliokuwepo na majambazi.
Hakika polisi walizidiwa nguvu kwani maiti zilikua nyingi sana majeruhi usiseme. Nikapanga vizuri vikosi kisa nikaamuru mashambulizi ya kiakili. Walinisikiliza na tukaendesha shambulio kwa mda wa dakika 15 bila mapumziko. Ndipo kimya kilitawala hapakua na risasi tena tokea upande wa pili yaani majambazi. Nikaamuru kuzingira eneo zima ili majambazi tuwaweke katikati. Walikua tayari wamezidiwa kwa kiasi kikubwa. Niliamuru mashambulizi tena huku nikiwaamuru maaskari wangu kusonga mbele. Mambo yalizidi kupamba moto mwisho tulikua tumefanikiwa kuua majbazi sita na wengine kuwajeruhi hawa walikua walwili. Wakatueleza ya kua walikua kumi hivyo wawili wamefanikiwa kutoroka. Niliamuru askari kadhaa tushirikiane kuwatafuta.
Shuhuli ya kuwatafuta ikaanza na kupamba moto. Kila mtu akatawanyika kila kona ili tuu tukamate majambazi. Nilifanya kazi kwa ufanisi sana. Nilisonga mbele. Lakini sikuona kitu. Mara kwa mbali nikamwona mtu akikimbia. Nikaanza kumfukuzia. Nilimfukuza sana. Yule mtu alikua akielekea upande wa barabara. Nikazidi kumfuata. Alipofika barabarani kumbe kulikua na pikipiki aliiacha huko. Akaikimbilia na kuiwasha. Chaajabu akawa haondoki. Nilizidi kumsogelea Mungu wangu alikuakua ni Zabroni Makweka nililijua hilo baada ya kumkaribia. Nikamlenga na bastola yangu kisha nikafyatua risasi________________________
EmoticonEmoticon