Ni
ajali nyingine iliyotokea Shinyanga na kuingia kwenye vitabu vya
kumbukumbu kwenye rekodi ya mwaka 2015 ikiambatana na nyingine nyingi
zilizoua Watanzania ikiwemo ile ya Basi lililowaka moto.
Ni saa tisa kasorobo Alasiri April 22 2015 ambapo Basi la abiria la Unique
aina ya Scania lililokua linaendeshwa na Issa Patrick (38) liligongana
na Trela ambayo dereva wake amekamatwa na Polisi sasa hivi.
Polisi Shinyanga imesema watu tisa ambao ni abiria wa basi walifariki hapohapo na mwingine mmoja akafariki baadae na majeruhi ni 51 ambao walipelekwa kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Chanzo cha ajali ni dereva wa lori aliekua anatokea Nzega kuelekea Shinyanga kuendesha gari katikati ya barabara
na akalishtukia basi wakati wameshakaribiana ambapo dereva wa lori
alichoweza ni kutoa kichwa cha lori tu barabarani lakini Trela
lililobaki kwenye barabara ndio likagongana na basi.
Kamanda wa Polisi amesema ni uzembe wa Madereva wote wawili kwa
sababu pia walikua kwenye mwendo kasi, unaweza kumsikiliza zaidi hapa
chini.
EmoticonEmoticon