Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
nchini TFF, Jamal Malinzi ametuma salamu za rambirambi kwa Rais wa Chama
cha Mpira wa Miguu cha Afrika Kusini (SAFA) Dr.Danny Jordan kufuatia
kifo cha nguli aliyewahi kuichezea timu ya Taifa ya nchi hiyo
(BafanaBafana) John Lesiba "Shoe" Mashoeu kilichotokea jana Aprili 21.
Katika salamau zake kwa Dr. Jordan,
Malinzi amesema nchi ya Afrika Kusini imepatwa na pigo kubwa katika
tasnia ya mpira wa miguu, kufuatia kifo cha Mashoeu aliyefariki dunia
kwa ugonjwa wa Kansa ya Utumbo, na kusema watanzania wako nao pamoja
katika kipindi hiki cha maombelezo.
John Lesiba "Shoe" Mashoeu aliyezaliwa
Disemba 18, 1965 nchini Afrika Kusini, alikuwa ni miongoni wa wachezaji
wa nchi hiyo waliotwaa Ubingwa wa Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) mwaka
1996 nchini Afrika Kusini na baadae kushiriki fainali za Kombe la Dunia
nchini Ufaransa mwaka 1998.
Wakati wa uhai wake Mashoe alipata
kuvichezea vilabu vya Giant Blackpool, Kaizer Chiefs, Amazulu na
Alexandria United vya Afrika Kusini, na timu Gencleribirligi,
Kocaeilispor, Fenerbahce na Busrsapor za Uturuki.
EmoticonEmoticon