Hussein Machozi ajiunga na ‘familia’ ya wasanii wajasiriamali, afungua kampuni yake ‘UTAIPENDA ENTERTAINMENT’


Katika hali ya kuonesha ukomavu wa kisanii hit maker wa “Kwaajili yako” Hussein Rashid a.k.a Hussein Machozi, ameamua kuungana na familia ya mastaa wanaomiliki kampuni zao binafsi kwa kuanzisha kampuni yake ya mambo ya burudani aliyoipa jina la moja ya nyimbo zake zilizowahi kufanya vizuri “UTAIPENDA ENTERTAINMENT”.
machozi-2
Akizungumza na Bongo5 Machozi amesema wazo la kuanzisha kampuni lilikuja baada ya kuona kuna baadhi ya mambo ambayo amekuwa akishindwa kufanya kutokana na kutokuwa na kampuni, ikiwa ni pamoja na kushindwa kupata deal za corporate na kupata wadhamini wa vitu vingi anavyokuwa anataka kufanya kama msanii.
“Unajua muziki jinsi ulivyo sasa hivi mtu kama mimi nategemea muziki kama source kubwa ya income na kikubwa zaidi nategemea shows sababu biashara ya albums kwa sasa hailipi bongo, sasa unakuta nashindwa kupata udhamini kwenye makampuni sababu wanakuwa wanaona hawawezi kudeal na mtu mmoja ila ni rahisi kama unakuwa na kampuni kabisa” Alisema Machozi.
Hussein Machozi ambaye kwa sasa ni baba wa mtoto mmoja wa kike aitwaye Zakia aliongeza kuwa Utaipenda Entertainment pia itakuwa inafanya vitu vya ziada lakini vyote vitakuwa vinahusiana na mambo ya burudani. Moja ya vitu hivyo ni kusaidia wasanii wachanga na wenye vipaji ambao watakuwa chini ya kampuni yake kama wafanyavyo wasanii kama AY kupitia kampuni yake ya Unity Entertainment na Mwana FA kupitia kampuni yake inayoitwa Lifeline Inc.
“Kwa sasa nina wasanii wanne lakini kati yao ni wawili ndio tayari tumeshaanza kufanya kitu, hawa wote ni wa Manyoni si unajua ndio home so nimeamua kuanzia nyumbani kwanza maana kule mzee kuna wasanii wengi sana wenye vipaji ila tu hawana njia ya kutokea, lakini baada ya Manyoni nitaenda mkoa mwingine” Alisema Hussein Machozi.
Moja ya hatua ambazo kampuni mpya ya Machozi imeshaanza kupiga ni pamoja na kuandaa show ya kumtafuta mrembo wa wilaya ya Bukombe mkoani shinyanga, Miss Bukombe inayotegemewa kufanyika June 1. Pia yuko katika mazungumzo na mapromota wa nchini Congo ambako muziki wa bongo fleva una mashabiki wengi sana kama ulivyoona ushahidi kupitia show ya Diamond hivi karibuni. “Saizi kuna show nimeandaa kupitia kampuni yangu ya Utaipenda Entertainment ni show ya Miss Bukombe inategemea kufanyika June 1, na kuna baadhi ya show za nje ziko on process”, Alisema Baba Zakia.
Kama haukua na taarifa Hussein Machozi ana mashabiki wengi sana nchi jirani ya Kenya (huenda zaidi ya Tanzania) ambako huwa anatumia muda mwingi kufanya shows huko zaidi ya Tanzania.
Mafanikio ya msanii yanaweza kupimwa kwa kupitia vitu mbali mbali moja wapo ikiwa ni shows anazopata, malipo anayolipwa kupitia show hizo, mauzo ya albums, mapato yatokanayo na biashara ya miito ya simu RBT (Ring back tones), mikataba ya kufanya kazi na makampuni (endorsement), lakini kubwa ni kupitia vitega uchumi binafsi ambavyo msanii mwenyewe anaweza kuwekeza, hivyo hongera  kwako Hussein Machozi kwa hatua nzuri
Previous
Next Post »