Askari wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora, H 3416 PC Charles, amejiua kwa kujipiga risasi.
Baadhi
ya wananchi wanaoishi jirani na kituo hicho cha polisi, Paulo Lazaro na
Furahisha Felix, walisema tukio hilo lilitokea Aprili 4, mwaka huu, saa
1:00 usiku kituoni hapo.
“Suala
hili limetushangaza, kwani sisi tulikuwa nyumbani. Ghafla tulisikia
mlio wa bunduki katika kituo cha polisi. Tulipofika, tulimkuta askari
huyo akiwa amekufa kwa kujipiga risasi,” alisema Lazaro.
Wananchi
hao walisema kutokana na hali hiyo, walilazimika kuwauliza baadhi ya
askari waliokuwa zamu, ambao walidai hata wao hawajui ni kwanini mwenzao
amechukua uamuzi wa kujiua.
Waliomba
ufanyike uchunguzi wa kina ili kubaini chanzo cha kujiua kwa askari
huyo kwani inawezekana kuna kitu ambacho alikuwa amechukizwa nacho.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Suzana Kaganda, alithibitisha kujiua kwa askari huyo. “Ni kweli askari huyo amejiua kwa kujipiga risasi wakati akiwa kituoni majira ya saa 1:00 usiku,” alisema Kamanda Kaganda.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Suzana Kaganda, alithibitisha kujiua kwa askari huyo. “Ni kweli askari huyo amejiua kwa kujipiga risasi wakati akiwa kituoni majira ya saa 1:00 usiku,” alisema Kamanda Kaganda.
Hata
hivyo, Kamanda Kaganda alisema hakuna ujumbe wowote ulioachwa na askari
huyo kuelezea sababu za kujiua. Kutokana na hali hiyo, Kamanda Kaganda
aliwataka askari wote kutatua matatizo yao kupitia kwa viongozi wao
badala ya kujichukulia sheria mkononi.
Alisema uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo cha askari huyo kujiua.
EmoticonEmoticon