Habari Zilizotufikia zinadai kuwa Mwenyekiti wa Jumuia ya wafanyabiasha nchini Tanzania Bwana Jonson Minja ameachiwa kwa dhamana na Mahakama ya Hakimu mkazi Mkoa wa Dodoma baada ya wafanyabiashara kuweka mgomo ambao ulikuwa haujafahamika ukomo wake.
Sakata
hili la wafanyabiashara kufanya mgomo wa kufunga maduka katika mikoa
mbalimbali nchini, jana lilichafua hali ya hewa bungeni baada ya baadhi
ya wabunge kuitaka Serikali itoe tamko kuhusu hali hiyo.
Tukio hilo liliibuka bungeni Mjini Dodoma jana baada ya kipindi cha maswali na majibu ambapo wabunge waliomba mwongozo ili kuhoji hali inayoendelea nchini dhidi ya baadhi ya wafanyabiashara kufunga maduka.

Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda na Biashara ambaye pia ni
Mbunge wa Kisesa, Wilaya ya Meatu, mkoani Simiyu, Luhaga Mpina,
alishangazwa na kauli zinazotolewa na Serikali kuwa mambo yao na
wafanyabiashara yako sawa badala ya kueleza walichojadili na kufikia
makubaliano.
"Waziri wa Fedha (Saada Mkuya), amekuwa akihudhuria katika vikao hivyo, kusikiliza hoja zao hivyo tunachokitaka alieleze Bunge hili suala linaloendelea si kusema uongo.
"Mwaka 2014 Serikali iliunda Kamati ya Maridhiano ambayo ilishirikisha wafanyabiashara waweze kukaa pamoja na Serikali kujadili na kufikia mwafaka lakini imechukua muda mrefu kuitisha vikao ili kujadili kwa pamoja," alisema.
Alisema hata wakiitisha vikao hivyo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara hao hayupo; hivyo itakuwa kazi bure na
kuitaka Serikali iangalie namna ya kumpatia dhamana kiongozi huyo ili vikao hivyo viendelee.

huyo anakabiliwa na mashtaka mawili ya kuwachochea wafanyabiashara
mkoani Dodoma kutenda kosa na kuwakataza wafanyabiashara nchini
wasitumie mashine za kieletroniki za kukusanya kodi za EFDS ambavyo
vyote ni makosa ya jinai.
Endelea kuwa nasi kwa habari motomoto.
Endelea kuwa nasi kwa habari motomoto.
EmoticonEmoticon