TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS
RELEASE” TAREHE 08.04.2015.
·
MWANAMKE MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA NGWALA
WILAYANI CHUNYA AUAWA KWA KUCHOMWA KISU NA MKE MWENZA.
·
MTOTO WA MIAKA MITATU AFARIKI DUNIA BAADA YA
KUGONGWA NA MKOKOTENI JIJINI MBEYA.
·
JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LINAWASHIKILIA WATU
SITA KWA MAKOSA MBALIMBALI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MWANAMKE MMOJA
MKAZI WA KIJIJI CHA NGWALA WILAYANI CHUNYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ELIZA SWEETY (44) ALIUAWA KWA KUCHOMWA KISU SEHEMU ZA SHINGONI, MGUU NA MKONO WA
KUSHOTO NA MKE MWENZA WAKE AITWAE PAULINA
EFESTI MWAMBE (46) MKAZI WA
NGWALA.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 06.04.2015
MAJIRA YA SAA 20:00 USIKU HUKO
KATIKA KIJIJI NA KATA YA NGWALA, TARAFA YA SONGWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA,
CHANZO CHA TUKIO HILO NI WIVU WA KIMAPENZI KWANI PAULINA EFESTI MWAMBE AMBAYE NI MKE MWENZA ALIKUWA AKIMTUHUMU
MAREHEMU KUPENDWA ZAIDI NA MUME WAO AITWAE GERVAS
MWAIPOSI (50) MKAZI WA NGWALA.
MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA UPELELEZI ZAIDI UNAENDELEA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTOTO MWENYE
UMRI WA MIAKA 03 ALIYEFAHAMIKA KWA
JINA LA AIRICH JACKSON MKAZI WA
IGAWILO ALIFARIKI DUNIA WAKATI ANAPATIWA MATIBABU KATIKA KITUO CHA AFYA IGAWILO
BAADA YA KUGONGWA NA MKOKOTENI.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 07.04.2015
MAJIRA YA SAA 15:30 ALASIRI HUKO
IGAWILO, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA
AJALI KINACHUNGUZWA. MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO. JITIHADA ZA
KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
TAARIFA ZA MISAKO:
KATIKA
MSAKO WA KWANZA, JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WANNE
WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. VICTOR EDGAR (24) MKAZI WA ILEMI 2. JAMES PASCHAL (21) MKAZI WA PAMBOGO 3. RULES KAJIGILI (27) MKAZI WA
MAKUNGULU NA 4. IKE MWAKYAMBIKI (30)
MKAZI WA MAKUNGULU WAKIWA NA BHANGI KETE
35 NA MISOKOTO 24 SAWA NA UZITO WA
GRAM 295.
WATUHUMIWA
WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 07.04.2015
MAJIRA YA SAA 13:30 MCHANA KATIKA
MSAKO ULIOFANYIKA HUKO ENEO LA MAKUNGULU, KATA YA RUANDA, TARAFA YA SISIMBA,
JIJI NA MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KATIKA
MSAKO WA PILI, JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA
MKAZI WA MAPELELE ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MARTHA FUNGO (60) AKIWA
NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA
03 NA MTAMBO MMOJA WA KUTENGENEZEA POMBE HIYO.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 07.04.2015
MAJIRA YA SAA 08:00 ASUBUHI KATIKA
MSAKO ULIOFANYIKA HUKO ENEO LA MAPELELE, KATA YA NSALALA, TARAFA YA USONGWE,
WILAYA YA KIPOLISI MBALIZI, MKOA WA MBEYA.
KATIKA
MSAKO WA TATU, JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA
MKAZI WA ILEMBO ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FRANK
JOHN (34) MVUVI AKIWA NA NYAVU
ZA KUVULIA SAMAKI AINA YA KOKOLO ZILIZOPIGWA MARUFUKU KUVULIA SAMAKI KATIKA
ZIWA RUKWA.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 07.04.2015
MAJIRA YA SAA 08:00 ASUBUHI KATIKA
MSAKO ULIOFANYIKA HUKO KATIKA KIJIJI CHA ILEMBO, KATA YA GALULA, TARAFA YA
SONGWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI
WATUHUMIWA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA NA POMBE MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI
HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA WAVUVI KUACHA KUTUMIA NYAVU
ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA
MAENDELEO YA VIUMBE VYA MAJINI.
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon