MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.
Sim no,0755683295/WatSap, Email@yusuphngahala@gmail.com.
SEHEMU YA KUMI NA TATU.
Tulipoishia Akamaliza na kuichomoa kisha akavaa kofia na kuondoka zake. Hakika nilizidiwa ujanja. Nilianza kuhisi mabadiliko ya mwili palepale. kwani nilihisi____Endelea... Nakauka damu. Nilijikuta napiga kelele za kuomba msaada akaingia Peris na kuniangalia. Nilikua tayari nimekauka mithili ya ukuni mkavu. Sauti ikaanza kukwama. Peri akatoka na kuja na daktari. Aliponiona tuu akamtuma nesi alete drip la damu haraka. Hata haikupimwa ni kundi gani kwani kufanya hivyo ilikua ni kupoteza mda. Akanitundikia drip kisha akanidunga sindano fulani. Sikujua nini kilijiri hadi pale niliposhtuka nikiwa na hali nzuri kiasi. Wakati nafumbua macho nilimwona Peris yuko pale na Anthony wakilia. Nilijitambua ya kua mimi ni mtu mwenye thamani sana. Peris alipoona nimefumbua macho alishindwa kuzuia hisia zake. Aliinama na kunibusu mdomoni mara kadhaa.
Anthony akafuta machozi. Niliumia sana kumwona Anthony analia kiukweli. Mtoto mdogo kama yule aliumia kwaajili yangu nlikua kama niliyepandikizwa gunia la hasira. Peris akatoka na kwenda kumwita daktari. Akaja na kuniangalia kisha akashauri nihamishiwe chumba cha siri. Baada ya kuhamishwa na siku kadhaa kupita hali yangu ilikua nzuri kabsa. Japo nilibaki na makovu ya kumwagiwa tindikali lakini sikujali hilo. Zilipita wiki kadhaa nikifanyishwa mazoezi pale hospitali. Baada ya kua vizuri kabsa nikaruhusiwa kutoka. Nilipotoka hatua yangu ya kwanza ilikua kufikia ofisi za gazeti lile lililonichafua. Nilipofika nilimfuata mhariri mkuu. Nikamwuliza juu ya zile habari wamezipata wapi? Nilikua nimefura kwa hasira nilimkunja haswaa. Wakati anaanza kuongea ghafla kuna mwenzake akamshika begani. Mara jamaa akaanguka na kufa palepale. Hali ile ilinitisha na kuamua kumkamata yule jamaa. Chaajabu wakati napambana naye alikua akitumia sana pete yake.
Nikagundua ile pete inakitu. Nikamtageti vizuri kisha nikamkamata ule mkono wenye pete. Alipoona kazidiwa nguvu akajigusa na ile pete naye akapoteza maisha. Niliivua ile pete na kuiangalia ilikua na kimwiba flani cha kukunja na kukunjua. Nilitoka na kurudi nyumbani. Nilimkuta Peris yuko na Anthony. Kwakua nilikua bado sijatulia nikaenda kituoni kuona kama wameshafika ofisi zile za magazeti ili kuchukua maiti zile mbili. Pia nilikua naenda kuangalia ile pete ina nini. Baada ya kumwona mtaalamu wa pale ofisini Akanambia ile ni sumu kali sana. Hua inatumika na Wavietnam kuwaua Wamarekani. Wao hupaka kwenye mishale hivyo ukipatwa na mshale ule unakufa papo hapo.
Sasa sumu ya Vietnam Tanzania inafanya nini? Nikatoka na kumfuata mkuu mkuu. Alinipa pole kisha akasema nisiwe na shaka tayari taarifa zile wamezikanusha. Nikamshukuru kisha akanambia sasa inabidi niongezewe kikosi ili kuifanya kazi kwa ufanisi. Akaniletea maafisa upelelezi wanne. Wote walikua wametoka Marekani kwenye kozi za kipelelezi. Wa kwanza alikua Onesmo, Wa pili alikua Upendo, Watatu alikua Mwita, na wa nne alikua Khajara. Hivyo tukawa watu sita ukimjumuisha na Peris. Tulifahamiana pale kisha tukakubaliana tuanze kazi siku inayofuata.
Peris hakuwepo ila nilipaswa kumfikishia taarifa. Basi baada ya pale nilichukua baadhi ya dokumenti na mafaili yanayohusu wale majambazi. Nikatoka nlipofika nyumbani nakumbuka ilikua mida ya saa 12 jioni. Nilimkuta Peris sebuleni akiangalia Tv. Anthony hakuwepo nadhani alikua kalala. Peris alikaa kimtego sana. Nilijua alikaa vile baada ya kusikia gari inaingia. Nikamsalimia Akainua mguu na kuweka juu kama amekunja nne. Kisha akaitikia salama za utokako.
Nikajibu nzuri. Lakini macho yangu yalikua yakimtazama Peris na kugundua kua hakuvaa kitu zaid ya khanga. Hivyo wakati ameinua mguu nilipata kuona mbali sana kwani khanga ilikua imemwachia eneo kubwa. Tamaa ikanivaa. Hisisia zikanitawala. Mapenzi yakateka akili yangu. Sikujua nifanye nini. Basi Peris akasimama na kusema nikupokee.?
Mmmmh mmmmh Aaah eeeee Saaa saaa sawa tuu. Niliitikia kwa kujikanyaga. Akachukua "briefcase" na kuanza kuelekea kuviweka chumbani kwangu. Alitembea kwa maringo huku sehemu za nyuma zikiniacha mdomo wazi. Nikaamua kumfuata kwa nyuma. Alipofika akaweka juu ya kabati. Lakini wakati anatoa mkono kule juu khanga yake ikaanguka. Nikaona kifua chake kizuri, kilikua kimesimama kama mtoto aliyetoka kuvunja ungo.Kitovu chake kilinitamanisha Pale nilipomwangalia kiuononi Mungu wangu. Nikajikuta nameza mate. Wakati anainama kuokota khanga akili yangu ikahama kabisaa. Nikamfuata na kumshika mkono. Alijua ninachotaka akaonyesha ushirikiano hatimae amri ya sita ikavunjwa. Mimi na Peris tukawa Mtu na mpenzi wake.
Usiku ule ulikua usiku mzuri sana. Asubuhi tukaamka na kujiandaa kwenda kazini. Tulipofika kazi ziliendelea kama kawaida. Tulishauriana upelelezi wetu ufanyike kwa mda mrefu lengo ilikua kuwatia nguvuni wote. Mwezi wa kwanza ukapita kisha wa pili na zaidi wa tatu. Tulikua tunakaribia kukamilisha upelelezi. Kwa bahati mbaya Peris alikua tayari mjamzito hivyo ilibidi awe anashinda nyumbani. Nakumbuka siku ambayo tulipanga kwenda kukamilisha upelezi wetu na kuanza operation ya kukamata wote. Siku hiyo ilikua Ijumaa nilikua njiani naenda ofisi ya wizara ya Mawasiliano. Wakati nafika nikamwona mtu akiwa amevaa kiaskari kama mimi anatoka pale mlangoni.
Baada ya kumwangalia vizuri alikua ni yule mwanaharamu anayefanana na mimi. Nilipata hasira Zabroni Zabroni! Nikashuka haraka kwenye gari. Mara naye akaingia kwenye gari na wakatoweka. Nikaingia kule kwenye ofisi za mawasiliano. Wakati nasukuma mlango nilikutana na Dimbwi la damu. Nikahamaki na kurusha macho mbele ambapo sikuamini ninachokiona. Wafanyakazi wote kila mtu kwenye kompyuta yake. Walikua wamekatwa vichwa na kuachwa pale.
Mle ndani ilikua ni bahari ya damu. Nilikua nikitembea juu ya damu. Nikawa nashangaa sana hali ile ilikua inatisha sana. Nikasogea huku na huko na kuona kama kuna yeyote yuko hai. Hapakua na dalili yoyote ya mtu kua hai. Nikawa najaribu kuangaza macho lakini wapi? Hao pekee walipaswa kutupa ushahidi wa mwisho je tutaupata wapi? Zabroni alikua ni mjanja na mwerevu kupindukia. Bahati mbaya nilisahau kupiga simu kituoni. Ghafla nikasikia king'ora cha gari za polisi zikija. Kwa vyovyote vile mimi ndo nitakamatwa mle ndani. Kosa ni kua sikutoa taarifa hivyo watasema mimi ndiye muuaji wa watu wote wale. Nikiwa nimeduwaa. Mara polisi waliingia na kuniweka chini ya ulinzi. Nikafungwa pingu na kupakiwa kwenye difenda kupelekwa kituoni kujibu tuhuma za mauaji._______________________
EmoticonEmoticon