Mwenyekiti
mtendaji wa IPP DR. REGINALD MENGI ameeleza kushtushwa na taarifa
zilizochapishwa kwenye gazeti la taifa imara zikimtuhumu kuwa ana nia
ya kutaka kuiangusha serikali ya Rais Kikwete na kumshughulikia baada
ya kumaliza muda wake wa uongozi kunyamaziwa na ikulu na idara ya
habari maelezo kwa wiki tatu bila kutoa ufafanuzi wowote.
Katika kauli yake kwa vyombo vya habari Dr. Mengi amesema
taarifa ya Gazeti hilo iliyouliza swali ,ZITTO AMCHONGEA MENGI KWA
JK ambayo pia imesema Rais Kikwete aliapa kupambana naye inampa hofu
kubwa kuhusu mustakabali wa maisha yake kutokana na kuachwa kuendelea
kusambaa kwa tuhuma hizo.
Amesema ukubwa wa hofu hiyo ni kutokana na Rais ambaye ni mkuu wa
majeshi ya ulinzi na usalama kauli yake kama ilivyonukuliwa na
Gazeti kuwa atapambana naye inaweza kuchukuliwa kama agizo kwa vyombo
vya dola kumuangamiza.
EmoticonEmoticon