Msanii wa Bongo Fleva,Hussein Machozi amefunguka na kusikitishwa na habari zilizoenea kuwa amefariki dunia baada ya kupata ajali ya gari mkoani Dodoma.
Alisema kuwa tangu habari hizo kuenea siku ya jana amekuwa akipigiwa sana simu na watu tofautitofauti wakimuuliza kama mzima wa afya. ‘’Jana nilikuwa nimezima simu kwa muda mrefu nilikuwa nimeenda mazoezini baada ya kurudi nilipowasha tu simu ziliingia kama mvua kilichonishangaza wengi walikuwa wakipiga wakisikia sauti yangu wanakata simu,’’alisema Hussein Machozi.
‘’Yaani kuna watu wamenipigia simu ambao walikuwa walishakata mawasiliano na mimi muda mrefu na nimeambiwa nyimbo zangu zimepigwa sana siku ya jana baada ya taarifa hiyo kuzagaa,’’aliongeza Hussein Machozi.
Aidha aliongeza kuwa ameamini kuwa msanii akishakufa thamani yake inaongezeka sana,na anatarajia kufanya dua na kualika watu mbalimbali nyumbani kwao kwa ajili ya kujiombea kutokana na tukio hilo
EmoticonEmoticon