Zitto Kabwe Akanusha taarifa za Kufukuzwa uanachama Ndani ya Chadema


Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe  Amefunguka muda huu kukanusha  juu ya tetesi za Kufukuzwa kwake uanachama ndani ya chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema kama ambavyo zimekuwa zikisambaa katika mitandao mbali mbali ya kijamii kufuatia muda mchache uliopita Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam kutupilia mbali Zuio lake la kujadiliwa na vikao vya  chadema ambapo ametakiwa kulipa gharama za kesi.

Zitto Kabwe amesema kuwa yeye mpaka wakati huu hana taarifa Rasmi na naendelea na kazi zake  kama kawaida” leo nilikuwa na EWURA,ratiba yangu inaonyesha kuwa kesho ntakuwa na TANNESCO,Na ratiba yangu inaonyesha kesho kutwa nashughulikia suala la mabilioni ya USWIZI ambapo mwanasheria mkuu wa serikali kamshina GENERAL wa TRA na Bei Gavana wa benki kuu anakuja mbele kujieleza kuhusu jambo hilo.Alisema Zitto Kabwe.

Amesema kuwa kwa upande wake hadi hivi sasa hawezi kuzungumzia chochote kwakuwa yupo safarini na taarifa hizo amezipata pia kupitia mitandao ya kijamii ikiwa imepost”Taarifa rasmi sina na siwezi kusema chochote mpaka niweze kupata taarifa rasmi,Wanasheria wangu tayari  wamekwenda mahakamani kwaajili yakuweza kupata hiyo JUDGEMENT na kuweza kuona nitaarifa zipi zitakazo fuata kwenye hiyo JUDGEMENT”Alisema Zitto kupitia Mazungumzo kwa Njia ya Simu.
Previous
Next Post »