Na RFI
Watu kumi
ikiwa ni pamoja na raia wanane wa Ufaransa wamefariki katika ajali ya
helikopta iliyotokea katika mkoa wa La Rioja, nchini Argentina.
Miongoni
mwa waliofariki ni pamoja na Florence Arthaud, bingwa wa michezo ya
kuogelea ya olimpiki Camille Muffat na mwanamisumbi Alexis Vastine.
Mabingwa
hao watatu wamekua wakishiriki pamoja na wanariadha wengine wa Ufaransa
katika utengenezaji wa makala ya " télé-réalité", ambayo ni mchezo mpya
wa kusisimua wa televisheni ya Ufaransa TF1.
Watu wote
hao kumi waliofariki walikua katika helikopta mbili walizokua wakitumia
katika kazi yao hio, ambazo ziligongana, kwa mujibu wa viongozi wa mkoa
wa La Rioja.
Wanamemba wa timu nzima ya Adventure Line Production, kampuni inayotengeneza yake.
Kwa
mujibu wa mwandishi wa RFI, katika mji wa Buenos Aires, Jean-Louis
Buchet, ajali hiyo imetokea saa kumi na moja jioni saa za Argentina
(sawa na saa mbili usikusaa za kimataifa), katika mkoa wa La Rioja,
kwenye umbali wa kilomita 2000 kaskazini magharibi mwa mji mkuu wa
Argentina, Buenos Aires. Helikopta hizo zilikua zikitokea katika kijiji
cha Villa Castelli, katika eneo la Andes.
Inaarifiwa kua helikopta hizo ziligongana baada ya kuruka kwenda juu kwenye umbali wa mita 100. Picha za ajali hiyo zinatisha.
Saa moja
baadae, polisi ya moka wa La Rioja ilitoa taafa kwamba hakuna mtu
aliyenusurika katika ajali hiyo. Marubani wawili kutoka Argentina wote
wamefariki.
EmoticonEmoticon