UMOJA WA WAFANYAKAZI NA WAUGUZI HOSPITALI YA RUFAA MBEYA NA WANANCHI WAMKABIDHI MSAADA KWA MAMA WA BARAKA MLEMAVU WA NGOZI.













Shah akiwa amembeba Baraka 
Umoja wa wafanya kazi na wauguzi wa hospitali ya Rufaa Mbeya pamoja na wananchi wamekabidhi msaada kwa mama wa mtoto Baraka mlemavu wa ngozi (albino) aliyekatwa kiganja mkoani Rukwa mwishoni mwa wiki iliyopita.
Misaada iliyotolewa na pesa tasilim shilingi laki nne, mavazi pamoja vyakula. Akizungumza na waandishi wa habari wafanyakazi hao wameiomba serikali kuchukua hatua kali kwa watu wanaowafanyia ukatili watu wenye ulemavu wa ngozi maarufu kama maalbino ambazo zitaweza kukomesha ukatili huo nchini Tanzania na kuhimiza kutendewa kazi kwa kauli mbiu ya 'MAUAJI YA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI (ALBINO) SASA IMETOSHA'


 Pamoja na hayo mkurugenzi wa hospitali ya Rufaa Mbeya, ndugu Ulusubisya Mpoki amewashukuru wananchi waliojitolea kutoa msaada wao wa hali na mali kwa wahanga wa tukio hilo pamoja na wauguzi waliojitolea kumuuguza wahanga mpaka sasa ambapo hali zao zinaridhisha.


 Kufuatia tukio hilo mama wa mtoto Baraka aliyejeruhiwa ametoa shukrani zake za dhati kwa wote walioguswa na matatizo yao lakini pia mama huyo ambaye kwa sasa ni mjamzito na anae mtoto mwingine mdogo ambaye pia yuko hospitali ameonesha hofu ya kurudi kijijini kwake kutokana na balaa lililompata mwishoni mwa wiki iliyopita.
Previous
Next Post »