JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WAGANGA KWA TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA VITENDO VYA UPIGAJI RAMLI CHONGANISHI.




TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 13.03.2015.

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WAGANGA KWA TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA VITENDO VYA UPIGAJI RAMLI CHONGANISHI.

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WAGANGA WANAOTUHUMIWA NA VITENDO VYA UPIGAJI WA RAMLI CHONGANISHI BAADA YA KUFANYIKA MSAKO MAALUM KATIKA WILAYA MBALIMBALI KATIKA MKOA WA MBEYA.

KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 06.03.2015 MAJIRA YA SAA 12:55 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA MTANILA, KATA YA MTANILA, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA, WALIKAMATWA WAGANGA WAPIGA RAMLI CHONGANISHI AMBAO NI 1. HAMIDU MIRAJI (41) MKAZI WA MTANILA AKIWA NA VIBUYU 6 NA KONOKONO WA BAHARINI 02 2. DORIS ELIA MWASELELA (42) MKAZI WA MTANILA AKIWA NA NGOMA 5 NA KITAMBAA CHEUPE (KIOO) 3. CHANDE SIMON (43) MKAZI WA MTANILA AKIWA NA KITAMBAA CHEUPE [KIOO] NA FIMBO NYEUSI 4. ARON MWASININI (70) MKAZI WA MTANILA AKIWA NA KITAMBAA CHEUPE (KIOO) NA 5. DICKSON MWAIGAGA (37) MKAZI WA KIBAONI AKIWA NA ZANA ZA UGANGA KITAMBAA CHEUPE [KIOO].

WATUHUMIWA WAMEFUNGULIWA KESI NA KUFIKISHWA MAHAKAMANI.

            AIDHA KATIKA MISAKO ILIYOFANYIKA MNAMO TAREHE 06.03.2015 NA 07.03.2015 MAJIRA YA SAA 09:00 ASUBUHI NA SAA 18:00 JIONI HUKO KATIKA KIJIJI CHA MKUTANO, KATA YA NZOKA, TARAFA YA NDALAMBO NA ULE ULIOFANYIKA MAENEO YA CHAPWA, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA.

           WALIKAMATWA WAGANGA WAPIGA RAMLI CHONGANISHI AMBAO NI 1. NOELIA LUSAMNBO (40) MKAZI WA MKUTANO  AKIWA NA VIPANDE VIWILI VYA NGOZI YA CHUI, KITAMBAA KIMOJA CHEUPE [KIOO], KUCHA ZA CHUI, MSALABA NA BIBLIA MOJA NA 2. EDWNI MWAMBUGI (60) MKAZI WA CHAPWA AKIWA NA VIBUYU 02, MKIA WA FARASI, PEMBE 04 ZA NG’OMBE, KIPANDE CHA NGOZI YA CHUI, SHANGA KWENYE KIBUYU, MIFUPA YA WANYAMA WA AINA MBALIMBALI WA PORINI, KIPANDE CHA NUNGUNUNGU NA BIBLIA YA KINYASA. WATUHUMIWA WAMEFUNGULIWA KESI NA KUFIKISHWA MAHAKAMANI.

         



             KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 07.03.2015 MAJIRA YA SAA 02:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA HALUNGU, KATA YA HALUNGU, TARAFA YA ITAKA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA. ALIKAMATWA MGANGA MPIGA RAMLI CHONGANISHI AITWAYE ABRAHAM KAPELELA @ SIMKOKO (65) MKAZI WA HALUNGU AKIWA NA MBWA MDOGO ALIYEKAUSHWA KWA MOSHI, MIKIA 05 YA PAKA PORI, PEMBE 03 ZA DIGIDIGI, MGUU 01 WA NYANI, MGUU 01 WA NDEGE AINA YA TAI, MGUU 01 WA MNYAMA AINA YA NYEGERE PAMOJA NA MADAWA MBALIMBALI YA MITI SHAMBA.
        
          UPELELEZI UNAENDELEA KUSHIRIKIANA NA OFISI YA MALIASILI KUBAINI THAMANI HALISI YA NYARA HIZO. HATA HIVYO MTUHUMIWA ALIFIKISHWA MAHAKAMANI TAREHE 12.03.2015.

KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 06.03.2015 MAJIRA YA SAA 07:00 ASUBUHI HUKO KATIKA MAENEO MBALIMBALI YA JIJI LA MBEYA KATIKA TARAFA ZA SISIMBA NA IYUNGA, MKOA WA MBEYA.

WAGANGA WAPIGA RAMLI CHONGANISHI WASIOKUWA NA VIBALI WALIKAMATWA AMBAO NI 1. MAFTAH SEBA (51) MKAZI WA MWAKIBETE 2. GADNER MWAKASYUKA (44) MKAZI WA KABWE 3. MAJESHI CHAWINGA (44) MKAZI WA ILOMBA 4. MSAFIRI NANGALE (44) MKAZI WA NJIA PANDA VETA.  5. MFIKEMO MWANAMAULA (50) MKAZI WA SHEWA NA 6. ANDREW KAYANGE (22) MKAZI WA SAE. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.


Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Previous
Next Post »