·
MTU MMOJA AMBAYE HAJAFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI
YAKE AUAWA NA WATU WASIOFAHAMIKA.
·
MWENDESHA PIKIPIKI AFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA
YA KUGONGWA NA GARI WILAYANI CHUNYA.
·
MTU MMOJA MKAZI WA IDIMI JIJINI MBEYA
ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA AKIWA NA MICHE 08 YA BHANGI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA AMBAYE HAKUWEZA KUFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI
YAKE, JINSI YA KIUME, UMRI KATI YA MIAKA
35 – 40 ALIKUTWA AMEUAWA NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA NA MWILI WAKE UKIWA
UMETELEKEZWA NDANI YA MTO MOMBA.
MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA MNAMO TAREHE 29.03.2015 MAJIRA YA SAA
08:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KITONGOJI, KIJIJI, KATA NA TARAFA YA KAMSAMBA,
WILAYA YA MOMBA MKOA WA MBEYA. MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA UKIWA UMEHARIBIKA
SANA HUKU UKIWA NA MAJERAHA YA KUKATWA KITU CHENYE NCHA KALI SEHEMU YA
KICHWANI, MIGUUNI, KIFUANI NA TUMBO KUPASUKA. CHANZO CHA TUKIO KINACHUNGUZWA.
JUHUDI ZA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI
ZINAENDELEA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KITUO CHA AFYA TUNDUMA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MWENDESHA PIKIPIKI MMOJA AMBAYE HAKUWEZA KUFAHAMIKA
JINA WALA MAKAZI YAKE, UMRI KATI YA MIAKA
25 – 30 ALIYEKUWA AKIENDESHA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.519
CRD AINA YA T-BETTER ALIFARIKI
DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA
GARI LISILOFAHAMIKA LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA
MAKAZI YAKE.
AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 29.03.2015 MAJIRA YA SAA
21:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA ISENYELA, KATA YA MBUGANI, TARAFA YA
KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA MBEYA/CHUNYA.
CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA WA GARI ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA
AJALI. JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA MATUKIO HAYO
AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE
DHIDI YAO.
TAARIFA ZA MISAKO:
KATIKA MSAKO WA KWANZA, JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA
MKAZI WA IDIMI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MICHAEL
JONAS (35) AKIWA NA MICHE NANE [08] YA BHANGI ALIYOPANDA ENEO LA NYUMBA YAKE.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 29.03.2015 MAJIRA YA SAA
17:00 JIONI HUKO KATIKA KIJIJI CHA IDIMI, KATA YA IHANGO, TARAFA YA
TEMBELA, WILAYA YA KIPOLISI MBALIZI, MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUMFIKISHA
MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUJIHUSISHA NA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA KWANI
NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon