·
MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA
BARABARANI WILAYANI RUNGWE.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA
WATU WAWILI KWA TUHUMA MBALIMBALI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA MKAZI WA JIJINI MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA
LA PETTER AMEDEUS MKUMBUKWA (37)
MENEJA MAUZO KAMPUNI YA MOHAMED ENTERPRISES CO.LTD TAWI LA MBEYA ALIFARIKI
DUNIA BAADA YA GARI WALILOKUWA WAKISAFIRIA LENYE NAMBA ZA USAJILI T.784 DCA AINA YA SHANDON LILILOKUWA
LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE JUMA
ALUKAMBA KULIGONGA KWA NYUMA GARI T.928
CKK AINA YA FUSO LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA LIFU MAHENGE.
AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 25.03.2015 MAJIRA YA
SAA 14:40 MCHANA HUKO KATIKA ENEO LA KIJIJI CHA IDWELI, KATA YA ISONGOLE,
TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA
MBEYA/TUKUYU.
AIDHA KATIKA AJALI HIYO, DEREVA WA GARI LENYE NAMBA T.784 DCA AITWAYE JUMA ALUKAMBA ALIJERUHIWA NA AMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA MISHENI
IGOGWE. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA GARI NAMBA T.784 DCA. DEREVA WA FUSO ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO, JUHUDI ZA
KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI
PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA/KANUNI NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA
AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
TAARIFA ZA MISAKO:
KATIKA MSAKO WA KWANZA, MTU MMOJA MKAZI WA MWAKAGANGA WILAYANI MBARALI
AITWAYE BARAKA NGAIRO (27),
ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE KALI
[VIROBA] ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI AINA YA BOSS PAKETI 45 NA VIPODOZI AINA YA BETASOL CREAM 112.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 25.03.2015 MAJIRA YA SAA 12:30 MCHANA HUKO ENEO LA
MWAKAGANGA, KATA YA UBARUKU, TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA
MBEYA.
KATIKA MSAKO WA PILI, MTU MMOJA MKAZI WA NZOVWE JIJINI MBEYA AITWAYE ESTON JACKSON (21), ANASHIKILIWA NA
JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA AKIWA NA NOTI BANDIA 18 ZA TSHS 5,000/= SAWA NA TSHS
90,000/= ZIKIWA NA NAMBA QW0894188
NOTI 11 NA AD6498390 NOTI 07.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 25.03.2015 MAJIRA YA SAA
14:00 MCHANA HUKO ENEO LA SOKOMATOLA, KATA YA SOKOMATOLA, TARAFA YA
SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA ALIKAMATWA AKIWA KWENYE HARAKATI ZA
KUTAKA KUWEKA PESA HIZO KWENYE AKAUNTI YA M-PESA DUKANI KWA SUNDAY CLEMENS (32) AFISA TAKUKURU, MKAZI WA NZOVWE. TARATIBU ZA KUMFIKISHA
MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUJIHUSISHA NA UINGIZAJI, USAMBAZAJI NA UUZAJI WA
BIDHAA [POMBE KALI] NA VIPODOZI VILIVYOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI KWANI NI
KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA, ANATOA WITO KWA
JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA ZA MTU AU MTANDAO WA WATU WANAOJIHUSISHA NA
UTENGENEZAJI NA USAMBAZAJI WA NOTI BANDIA ILI WAKAMATWE NA HATUA KALI ZA
KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon