
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS
RELEASE” TAREHE 16.03.2015.
MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA MITANO AUAWA
KWA KUKATWA KICHWA KWA SULULU NA MJOMBA WAKE.
MTOTO
MWENYE UMRI WA MIAKA 05 ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA JONSON MWAMWERE, MKAZI WA NSALAGA JIJINI MBEYA, ALIUAWA KWA KUPIGWA
SULULU KICHWANI NA KUTENGANISHWA KICHWA
NA KIWILIWILI NA MJOMBA WAKE AITWAYE YONA MWAMWERE (38) MKAZI WA NSALAGA.
TUKIO
HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 16.03.2015
MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI HUKO
KATIKA MTAA WA NSALAGA-UYOLE, KATA YA NSALAGA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA
WA MBEYA.
AWALI
INADAIWA KUWA, YONA MWAMWERE ALIKUWA
ANAMFUKUZA MTOTO HUYO AMBAYE NI MJOMBA WAKE KUTOKA NYUMBANI NA ALIKIMBILIA
KWENYE JENGO LILILOPO JIRANI NA NYUMBANI KWAO AMBALO BADO LIPO KWENYE UJENZI.
HATA
HIVYO TAARIFA ZINADAI KUWA, YONA
MWAMWERE ALIPOFIKA KWENYE JENGO HILO ALIWATISHIA MAFUNDI WALIOKUWA
WANAJENGA NA WOTE WALIKIMBIA, HIVYO ALIMUUA MJOMBA WAKE HUYO KWA KUMPIGA
KICHWANI KWA SULULU NA KUTENGANISHA KICHWA NA KIWILIWILI.
KUFUATIA
TUKIO HILO MAFUNDI WALIOKUWA WAKIENDELEA NA UJENZI WALIPIGA KELELE ZA KUOMBA
MSAADA, HIVYO KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI
WALIJITOKEZA NA KUMSHAMBULIA MTUHUMIWA KWA KUMPIGA HADI KUFA NA KISHA KUUCHOMA
MOTO MWILI WAKE.
MAREHEMU
WOTE WALIKUWA NI NDUGU WANAOISHI NYUMBA MOJA, MIILI YAO IMEHIFADHIWA HOSPITALI
YA RUFAA MBEYA. CHANZO CHA TUKIO HILI KINACHUNGUZWA INGAWA UCHUNGUZI WA AWALI
UNAONYESHA KUWA MAREHEMU YONA MWAMWERE
ALIKUWA NA MATATIZO YA AKILI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA POLE KWA FAMILIA
YA MAREHEMU KUTOKANA NA TUKIO HILO. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII/WANANCHI KUACHA
TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE
WAJENGE TABIA YA KUWAFIKISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA
TUHUMA MBALIMBALI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon