

Jeshi
la polisi mkoani Mbeya, limefanikiwa kurejesha hali ya utulivu kufuatia vurugu
zilizoibuka mapema leo asubuhi katika Mamlaka ya mji mdogo wa Tunduma na jeshi
hilo kulazimika kutumia nguvu, huku watu 26 akiwemo Diwani wa kata hiyo Frank
Mwakajoka kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za uchechezi.
Chanzo cha
tukio hilo ni kugombea eneo moja la wazi lililopo Sogea, linalodaiwa
kumilikiwa Chama Cha Mapinduzi kata hiyo, ambapo wananchi wanahitaji kujenga
zahanati huku CCM wakitaka kulitumia eneo hilo kwa matumizi mengine.
Habari
zimeeleza kwamba, ujenzi wa zahanati hiyo ulianza wiki iliyopita ambapo baada
ya kazi hiyo kuanza CCM walikwenda kupinga katika Baraza la kata ambalo
liliwapo ushindi ccm, ambapo wananchi hao walikata rufaa baraza la ardhi la
wilaya ambako walitupilia mbali dai hilo ndipo wakaanza kujenga kwa nguvu.
Mwenyekiti wa
kitongoji cha Sogea ambaye hajataja jina lake amesema wanachohitaji wananchi wa
Tunduma ni maendeleo na si vurugu kama ambavyo imetokea.
Mkurugenzi
Mtendaji wa mji wa Tunduma Juma Kitabuge akizungumza na Ilasi fm kwa njia ya
simu amesema kumbukumbu zinaonesha kuwa kiwanja hicho kinamilikiwa na CCM.
Amesema hata
hivyo ameagiza kwamba kwa kuwa eneo hilo limekuwa na mgogoro basi lisifanyiwe
shughuli yoyote hadi pale suala la msingi litakapofanyiwa kazi.
Kitabuge ameongeza
kuwa ofisi yake imeagiza kila mwananchi anapotaka kujenga jengo lolote hata
kama ni kiwanja chake aihusishe ofisi ya ardhi ili aruhusiwe na kwamba wananchi
nao hawakufuata taratibu ikiwa ni pamoja na Idara ya afya.

Kwa upande wao
viongozi wa CCM hawakupatikana na kuwa ofisi zao zimefungwa ikidaiwa kuwa wapo
ziarani vijijini.
Kwa upande wake
katibu wa chadema wilaya ya Momba Godfrey Siame akizungumza na kituo hiki
amesema amesikitishwa na tukio hilo na kusema kwani jambo lililokuwa
likifanyika ni kwaajili ya jamii na si kama lilovyochukuliwa kuwa ni la
kisiasa.
Kufuatia vurugu
hizo watu 26 wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya mbozi akiwemo diwani wa
kata ya Tunduma Frank mwakajoka(CHADEMA) na wamenyimwa dhamana hadi march 30
mwaka huu.
Imedaiwa mbele
ya hakimu wa mahakama ya wilaya Names Chami na mwendesha mashitaka wa polisi
Joel Mori kwamba washitakiwa kwa pamoja bila uhalali walifanya mkutano kinyume
cha kifungu 74 na 75, shitaka lingine ni kufanya fujo na kuchoma matairi
barabarani kinyume na kifungu 89 (1) B, Kuharibu mali kinyume cha kifungu 326
(1) na kushawishi watu kutenda kosa.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !