AJALI mbaya ya gari
imetokea asubuhi ya leo saa 3.30 Jumatano katika kijiji cha Changarawe wilayani
Mafinga mkoani Iringa baada ya basi la abiria la kampuni ya Majinjah lenye namba za usajili T438 CDE lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea Dar es
Salaam kugongana na lori la mizigo lililokuwa likitokea Dar kuelekea Mbeya na
kusababisha vifo vya watu wanaokadiriwa kufikia 41 na majeruhi 22.
Habari kutoka eneo la tukio,
zinasema ajali hiyo ilitokea wakati lori hilo lililokuwa limepakia kontena,
likiwa katika mwendo kasi lilipojaribu kulikwepa shimo lililokuwa
katikati ya barabara na lilipotaka kurudi upande wake, ndipo lilipogongana uso
kwa uso na basi hilo.
lnakadiriwa kuwa na zaidi ya abiria 50
walikuwa ndani ya basi hilo na baada ya
lori hilo kugongana na basi kontena lake
likaliangukia basi kiasi kwamba abiria wote wamelaliwa watu wengine wanadaiwa walirushwa katika
korongo kufuatia kishindo cha mgongano.
Watu ni wengi katika eneo la tukio na miongoni mwao ni viongozi wa serikali Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Juma
Masenz,Kamanda wa Polisi mkoani humo Ramadhani Mungi .
Katika ajali hii pia mwanahabari mwenzetu Mercy Mwalusamba amempoteza mtoto wa mama yake mdogo kijana wa kiume ambaye alikuwa katika basi.
Bado tunasubiri taarifa kamili kutoka kwa Kamanda wa Polisi mkoani humo Ramadhani Mungi
Mtandao huu unatoa pole kwa
majeruhi na wafiwa wote.
EmoticonEmoticon