Gari aina ya Toyota Hilux ambayo imegongwa na Basi la Kampuni ya Majinja likiwa linatoka Mbeya kwenda Dar. |
Mwili wa marehemu ambae hakutambulika jina lake mara moja ukiwa katika Gari ya Polisi. |
(Picha na Fahari news)
Mtu mmoja amefariki dunia na wengine
zaidi ya 40 wamenusurika kifo katika ajali ya barabarani iliyotokea majira ya
saa 12:15 asubuhi njia panda ya Mafiati jijini Mbeya ikihusisha magari mawili
yaliyogongana uso kwa USO.
Ajali hiyo imehusisha basi la abiria mali ya
kampuni ya Majinja lililokuwa likielekea Dar es Salaam kutoka jijini Mbeya na
gari dogo ambalo halikufahamika Mara Moja.
kutokana na kuharibika sana ambalo dereva wake
amepoteza maisha pale pale na hakufahamika jina lake mara moja.
Pamoja na hayo shuhuda wa tukio hilo
ambaye ni mlinzi katika kituo cha Oilcom Mafiati amesema kuwa dereva wa basi la
Majinja ambaye hakufahamika kwa jina alikuwa akiendesha gari kwa mwendo kasi
kitu kilicho sababisha gari kumshinda na kuparamia gari do go lililokuwa
likitokea Mwanjerwa na kuharibika kabisa.
Taarifa tuliyoipata katika eneo la tukio ni
kwamba hakuna abiria yeyote aliyejeruhiwa kutoka katika basi hilo la abiria na
mwili wa marehemu ulichukuliwa na askari kwaajili ya uchunguzi zaidi.
CREDIT TO FAHARI NEWS |
|
Artikel Menarik Lainnya
TRA Yaja na Mikakati 5 Ukusanyaji Kodi. MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imeweka mikakati mitano ya kuboresha ukusanyaji kodi ya
Taarifa toka Ikulu: Rais Magufuli atoa tuzo CTI aahidi kuwaunga mkono wenye viwanda
VYAMA VYA UPINZANI KENYA WATANGAZA MGOMBEA ATAKAYESHINDANA NA RAIS KENYATTA KWENYE UCHAGUZI MKUU Muungano wa Vyama vya Upinzani nchi Kenya NASA umemtangaza mwanasiasa m
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa afanya ziara ya kushtukiza mabasi ya mwendo kasi
RAIS DKT. MAGUFULI AHUDHURIA KIKAO CHA UMOJA WA AFRIKA (AU) MJINI ADDIS ABABA ETHIOPIA Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Kati
Gari dogo limegonga basi la mwendo kasi (DART) katika makutano ya barabara ya Morogoro na Bibi Titi.
EmoticonEmoticon