TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA
WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 09.02.2015.
Ø WATU
WATATU WAFARIKI DUNIA NA WENGINE KUMI NA TATU WAJERUHIWA KATIKA AJALI WILAYANI
ILEJE.
Ø MTU
MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA GARI WILAYANI MBEYA.
Ø MWANAUME
MMOJA AMUUA MKE WAKE KISHA KUJINYONGA WILAYA YA MBEYA.
Ø MWANAUME
MMOJA AMUUA MKE WAKE KISHA KUMTUPA PORINI WILAYA YA MOMBA.
Ø MTU
MMOJA ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA UKATILI WA KIJINSIA DHIDI YA MTOTO WAKE
WILAYA YA MBOZI.
TUKIO LA KWANZA.
WATU WATATU WAFARIKI DUNIA NA
WENGINE KUMI NA TATU [13] KUJERUHIWA KATIKA AJALI YA GARI WILAYANI ILEJE.
WATU
WATATU WANAWAKE 1. ANNA MATWINZA [40] NA
WENGINE WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA JINA MOJA MOJA 2. EDINA NA 3. EDA, WOTE WAKAZI
WA AIRPORT MBEYA MJINI WALIFARIKI DUNIA
KATIKA TUKIO LA GARI KUACHA NJIA KUPINDUKA NA KUSABABISHA VIFO NA MAJERUHI.
TUKIO
HILO LIMETOKEA TAREHE 08.02.2015 SAA 20:00HRS KATIKA KITONGOJI CHA MAWELO,
KIJIJI CHA IZIRA, KATA YA IWAJI, TARAFA
YA BUNDALI BARABARA YA IYULA/ITUMBA.
KATIKA
TUKIO HILO GARI T.832 BKB AINA YA MITSUBISHI FUSO LIKIENDESHWA NA DEREVA AMBAYE
HAKUWEZA KUFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE LIKIWA LIMEBEBA MIFUKO YA SIMENTI NA
WATU KWA AJILI YA UJENZI KATIKA HOSPITALI YA SERIKALI WALAYA YA ILEJE LILIACHA
NJIA NA KUPINDUKA HIVYO KUSABABISHA VIFO HIVYO NA MAJERUHI KWA WATU WENGINE
KUMI NA TATU KATI YA YAO WANAWAKE NI NANE [08] NA WANAUME NI WATANO [05].
MAJERUHI
HAO NI PAMOJA NA 1. BAHATI MWAIKUMBILO [33], 2. IVA MWAIKUMBILO [33] 3. BROWN
TEMSON [32] 4. ANITA MTAVANGU [32], 5.MATRIDA AMOS [41], 6.AMINA ISAMAIL [46],
7.EVA KYOMA [44] 8.MONICA BENSON [33]. 9.GETRUDA GEHAZI [44] 10.DANIEL STAIN
[46] 11.JUMA DAUD [32] 12. PIUS GEORGE [30] NA 13. DORAJI BONIFACE [26] WOTE
WAKAZI WA MBEYA MJINI. MAJERUHI WAOTE WAMELAZWA HOSPITALI YA SERIKALI WILAYA YA
ILEJE KATI YAO WATATU HALI ZAO SIO NZURI.
CHANZO
CHA AJALI NI UTELEZI ULIOTOKANA NA MVUA KUBWA ILIYOKUWA IMENYESHA ENEO HILO.
DEREVA WA GARI HILO ALIKIMBIA NA KUTELEKEZA GARI ENEO LA TUKIO MARA BAADA YA
AJALI.
TUKIO
LA PILI
MTU
MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU JIJINI
MBEYA.
KATIKA
TUKIO HILO OSCA JAPHET SAGAJE [25],MKAZI WA ILEMI – MBEYA,ALIFARIKI DUNIA PAPO
HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LISILOFAHAMIKA AMBALO LILIKUWA LIKIENDESHWA NA
DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE.
TUKIO
HILO LILITOKEA TAREHE 08.02.2015 MAJIRA YA SAA 20:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA
MAKWENJE,KATA YA INYALA,TARAFA YA TEMBELA,WILAYA YA MBEYA VIJIJINI, KATIKA
BARABARA KUU YA MBEYA/IRINGA.
CHANZO
CHA AJALI HIYO BADO KINACHUNGUZWA. MTUHUMIWA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA
TUKIO.
TUKIO LA TATU.
MWANAUME
MMOJA AMUUA MKE WAKE KISHA KUJINYONGA
WILAYA YA MBEYA.
ZAINABU
GWANDUMBI [29],MKAZI WA MTAA WA ILOLO ALIKUTWA AMEUAWA NDANI YA NYUMBA KWA
KUPIGWA NONDO KICHWANI NA MUME WAKE ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA GWANDUMBI KIPENYA
[32], MKAZI WA MTAA WA ILOLO.
TUKIO
HILO LILITOKEA TAREHE 08.02.2015 MAJIRA YA SAA 09:00HRS KATIKA MTAA WA
ILOLO,KATA YA SINDE,TARAFA YA SISIMBA JIJINI MBEYA. MARA DAADA YA KUFANYA
MAUAJI HAYO MTUHUMIWA GWANDUMBI KIPENYA ALIINGIA CHUMBANI NA KUJINYONGA KWA
KUTUMIA MKANDA WA BEGI HADI KUFA.
CHANZO
CHA MATUKIO HAYO BADO KUFAHAMIKA KWANI
HAKUNA UJUMBE WOWOTE ULIOKUTWA NDANI YA NYUMBA HIYO.
TUKIO
LA NNE.
MWANAUME MMOJA AMUUA MKE WAKE KISHA KUJINYONGA WILAYA
YA MOMBA.
NGILO
NGINANZILWA [28],MKAZI WA WILAYA YA SHINYANGA VIJIJINI, ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUPIGWA
NGUMI KICHWANI KISHA KUNYONGWA SHINGO NA MUME WAKE ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JOHN
MANONI, [31]MKAZI WILAYA YA SHINYANGA VIJIJINI MKOA WA SHINYANGA.
TUKIO
HILO LILITOKEA TAREHE 07.02.2015 MAJIRA YA SAA 20:00HRS KATIKA KIJIJI CHA
SAZYA, KATA YA CHILULUMO, TARAFA YA KAMSAMBA.
CHANZO
CHA TUKIO HILO NI WIVU WA KIMAPENZI
ULIOTOKANA NA MGOGORO WA MUDA MREFU KATI YAO KUFUATIA MAREHEMU KUMYIMA MUME
WAKE KUFANYA TENDO LA NDOA.
MAREHEMU NA MTUHUMIWA WALIFIKA KIJIJINI HAPO NA KUFIKIA
NYUMBANI KWA SHANGAZI YAKE NA MAREHEMU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MWIGULU NEEMA
[54],MKAZI WA KIJIJI HICHO.
MTUHUMIWA
AMEKAMATWA NA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.
TUKIO
LA TANO.
MTU MMOJA ASHIKILIWA NA JESHI LA
POLISI KWA UKATILI WA KIJINSIA DHIDI YA MTOTO WAKE WILAYA YA MBOZI.
TABU LAISON MBAGWA [19],MKAZI WA
KIJIJI CHA IWEZI, ALIKUTWA AMEFUNGIWA NDANI YA MOJAWAPO YA VYUMBA VILIVYOPO
KATIKA NYUMBA YAO KIJIJINI HAPO NA BABA YAKE MZAZI JOHNSON SAIDIA MBAGWA [65],MKAZI WA KIJIJI CHA
IWEZI.
TUKIO HILO LILITOKEA TAREHE
08.02.2015 MAJIRA YA SAA 16:00HRS KATIKA KIJIJI CHA IWEZI,KATA YA IGAMBA.
KATIKA TUKIO HILO MHANGA AMBAYE ANA MATATIZO
YA AKILI NA KUANGUKA UGONJWA WA KIFAFA, ALIKUTWA AMEFUNGWA KAMBA MIGUUNI NA
KUNYANYAPALIWA KWA KUFUNGIWA CHUMBA MAALUM KWA MUDA WA MIEZI MIWILI HIVYO KUPELEKEA KUDHOOFU AFYA NA KUPELEKWA HOSPITALI YA
SERIKALI WILAYA YA MBOZI KWA MATIBABU. MTUHUMIWA BABA MZAZI WA MHANGA
AMEKAMATWA NA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WATUMIAJI WA VYOMBO VYA MOTO
KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA
KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI WALIPO
WATUHUMIWA [MADEREVA] WALIOSABABISHA AJALI HIZO WAZITOKE KATIKA MAMLAKA HUSIKA
ILI WAHUSIKA WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE,VINGINEVYO WAJISALIMISHE MARA
MOJA.
AIDHA
KAMANDA MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII HUSUSANI WANANDOA KUTATUA MATATIZO/KERO/MIGOGORO
YAO KWA NJIA YA MAZUNGUMZO BADALA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI INALETA
MADHARA MAKUBWA KWA JAMII NA HUSUSANI FAMILIA.
IMESAINIWA NA
[ AHMED Z. MSANGI – SACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon