Siku
chache baada ya kuzinduliwa kwa sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014
na Rais Jakaya Kikwete, chama cha NCCR mageuzi kimesema sera hiyo haina
manufaa yenye tija kwa wananchi bali sera hiyo imelenga uchaguzi mkuu
kwa kuwalaghai wapiga kura na sio kutekeleza yaliyomo ndani ya sera
hiyo.
Mwenyekiti
wa NCCR mageuzi taifa Mh James Francis Mbatia ameyabanisha hayo mbele
ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati akieleza masuala
mbalimbali yaliyoanishwa ndani ya sera mpya ya elimu ambayo imeandaliwa
kwa muda wa miaka saba hadi kukamilika kwake na kuzinduliwa Februari 13
mwaka huu na rais Jakaya Kikwete na kuanisha mpango wa serikali wa kutoa
elimu bure pindi sera hiyo itakapoanza kutumika jambo ambalo amelieza
kuwa ni kutendawili kisichokuwa na jibu kamwe.
Kuhusu
muda wa kipindi cha miaka saba kilichotumika kuiyandaa sera hiyo hadi
kukamilika kwake Mh Mbatia amesema ni muda mrefu umetumika huku sera
ikiwa imegubikwa makosa mengi ya uchapaji pamoja na kushindwa kwenda na
kasi ya mabadiliko ya teknolojia ya sasa duniani hivyo sera imeshapitwa
na wakati hata kabla haijaanza utekelezaji wake kwa wananchi.
EmoticonEmoticon