Baraza
la mitihani la tanzania limetangaza matokeo ya mtihani wa taifa wa
kidato cha pili kwa mwaka 2014 huku kiwango cha ufaulu kikiongezeka
kutoka asilima 89 hadi asilima 92 kwa mwaka 2014 ikiwa ni ongezeko la
asilimia 3.
Pamoja na kupanda kwa ufaulu wa jumla takwimu zinaonesha kuwa
ufaulu wa masomo ya sayansi yakiwemo hisabati na biashara upo chini ya
asilima hamsini hivyo juhudi za makusudi zinahitajika kuendelea
kufanyika ili kuinua kiwango cha ufaulu wa masomo hayo.
Kutokana na matokeo hayo walimu na wafunzi wametakiwa kuendeleza
juhudi katika ufundishaji na ujifunzaji katika masomo ambayo wanafunzi
wameonekana kutofanya vizuri waongeze juhudi kwa kipindi kijacho waweze
kufanya vyema.
EmoticonEmoticon