WENYEVITI walioychauliwa na wananchi na kuchukua hatamu za uongozi katika serikali za mitaa kupitia chama cha democrasia na maendeleo (CHADEMA) wilayani Momba mkoani Mbeya wametakiwa kufanya kazi kwa ajiri ya wananchi na sio masilahi binafsi.

 
 
Na  Saimeni mgalula, Momba- Mbeya

WENYEVITI  walioychauliwa na wananchi na kuchukua hatamu za uongozi
katika serikali za mitaa kupitia chama cha democrasia na maendeleo
(CHADEMA)  wilayani Momba mkoani Mbeya wametakiwa kufanya kazi  kwa
ajiri ya wananchi na sio masilahi binafsi.

Rai hiyo imetolewa na Mbunge wa jimbo la Mbozi Manghalibi David
Silinde(CHADEMA) Katika mkutano uliotishwa kwa ajiri kuwapa pongezi
wananchi  kwa kukiamini chama cha Democrasia na Maendeleo (CHADEMA)
kwa kupata ushindi wa kishindo kwa kuibwaga CCM kwa viti 48 kwa 23
katika mitaa 71 katika halmashauli ya mji mdogo wa Tunduma uliofanyika
katika uwanja shule ya msingi Tunduma.

Alisema kuwa ni wakati wa kuwajibika na sio kulala mpaka kieleweke
maana tunduma kulingana na mapato yake katika serikali kupitia kodi ya
wananchi  ya mapato na ushulu ipo juu lakini Tunduma katika huduma za
kijamii ni Mbovu.

‘’Kiongozi yeyote amabae kwa sasa kama alikuwa anagombea akizani
anaenda kunufaika kwa kupitia fedha ambazo ni kwa ajiri ya miundo
mbinu ya wanachi ameula bola achie ngazi mapema kabla hatujaindia
katika utendaji ‘’ alisema Silinde.

Alisema kuwa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA ) hakita
mvumilia kiongozi yeyote atakae tuhumiwa kwa ubadhilifu wa Fedha za
uendeshaji wa miundombinu kwa ajiri ya  maendeleo ya Wanatunduma.

‘’CHADEMA haiangalii wadhifa  na umalufu wa mtu inaangalia uwajibikaji
wa kiongozi kwa wananchi wake , mtu kama  unatumia mali za uma kuwa
mali binafi wewe kwetu ni mzigo hatuta chelewa kukuengua na
kusimamisha aliye tayali kuwawajibikia wapiga kula wake’’ alisema.

‘’Kumbukeni yale ya Aruhsa tuliwafukuza madiwani wa kata nne baada ya
kuona ni watovu wa nidhamu na haifuati ilani ya Chama Cha Democrasia
na maendeleo pia hawawajibiki ipasavyo’’  aliongeza.

Hata hivyo aliwata wananchi wa wilaya ya Mboma kuwa wavumilivu na
viongozi wao mala wakoseapo  kwa kuwakosoa na kuwaelekeza jinsi ya
kufanya  maana kila mwanadamu ana mapungufu na hajui vitu vyote
duniani .

Alisema kuwa sio kwamba mtu ukigombea na kupata wadhifa ndio unajua
uongozi,, hapana unaweza ukapata nafasi ya kuiongoza jamiii na
unaiongoza jamii ambayo ni zaidi ya kiongozi hivyo msisite kuwakosoa
viongozi wanao bugi ili gurudumu la maendele lisonge Mbele.

Pia aliwataka wananchi kuwavumilia viongozi wao katika kupanga na
kufanya shughuli za  maendeleo maana maendeleo ni mipango na hauwezi
kukuklupuka katika kufanya maendeleo .

‘’Kuna baadhi ya Wananchi kama umechaguliwa leo wanataka leoleo uanze
kufanya maendeleo katika maeneo yao , uwajibikaji haupo hivyo lazima
ujipange na uwe na mpangilio vininevyo uachemka’’ aliwataka wananchi.

Pia aliwata viongozi wote kuitisha mikiutano mala kwa mala na wananchi
wao ili kujua changamoto zinazo wakabili wananchi na kuziwasirisha
katika balaza ili zifanyiwe kazi na kuzitatua ili wananchi wawe na
imani na viongozi wao.

‘’Kaeni na wananchi sio kujifanyia shuli bila kuwahusisha wananchi
mipango yenu katika balaza lenu maana sas ni wakati wa kuleta
maendeleo kwa walipa kodi’’ alisema Silinde.
                                Mwisho
Previous
Next Post »