Na Lupakisyo
Kingdom ,Momba –Mbeya.
WANANCHI
katika mitaa ya Chipaka , Ndelema katika
mji mdogo wa Tunduma wilayani Momba mkoani Mbeya wamekerwa na na vitendo vya
baadhi ya walimu katika shule ya msingi Chipaka kuwa watoro na kurudisha nyuma mapango wa
serikali katika kutekeleza mpango wa matokeo makubwa sasa katika wizara ya Elimu.
Hayo yamesemwa
na baadhi ya wananchi wa katika mitaa hiyo walipokuwa wakizungumza na mwandishi wetu jana , walisema kuwa kuna baadhi ya
walimu wanaingia shuleni muda wa saa tatu na ifikapo saa sita wanapanada magari na kuludi makwao ambapo
ni nje ya utalatibu wa kazi yao.
‘’Tunajua
kuwa sheria na utalatibu wa shule zote za msingi Nchini ni kwamba walimu muda
wa kuingia shuleni ni saa mbili asubuhu na muda wa kutoka ni saa kumi jioni nje
na hapo kama kuna dhallula lakini kwetu yamekuwa kama maoea’’ alisema kijana
mmoja ambaye hakutaja jina.
Walisema kuwa
wanafunzi muda wa saa sita baada ya kuondoka kwa walimu baadhi na kubaki baadhi yao ambao wanafuata sheria za ajira yao nao wanafunzi
wanaamua kuludia makwao maana
wanabaki wanacheza bila kufundishwa.
‘’Endapo
wataendelea bila ya kuchukuliwa hatua basi mpango wa serikali ya jamhuli ya
muungano wa Tanzania wa matokeo makubwa sasa katika wizara ya elimu tusahau na
itabaki kuwa kauli mbiu isiyo kuwa na utekezaji’’ ,walisema.
Walisema
kuwa inaonekana kwa upande ya uondozi wa wilaya wanaonekana wameshindwa
kulitatua hili hivyo tuanamuomba waziri mwenye dhamana Shukulu Kawmbwa asikie
kilio cetu maana hasala ni kwa watoto wetu ambao wanaishia kuolewa.
Walisema kuwa
kuna baadhi ya walimu tumewahi kuwahoji na walicho chibu ni kwamba badhi
hawawezi kuwajibishwa maana ni marafiki
na badhi ya wafanyakazi katika ofisi za wiraya katika wizara ya Elimu.
‘’Usistajabu
kuona baadhi yao unawakuta katika shughuli binafsi muda ambao walistahili kuwa
dalasani kuwafundisha watoto wetu ambapo
wanajivunia kuwa wamesoma na maofisa elimu’’ walisema kwa uchungu.
Aidha baadhi
ya wanafunzi walisema kuwa hiyo inasababisha saana kupolomoka kwa elimu katika
shule hiyo ambapo kwa mwa huu walio hitimu shule ya msingi walikuwa wanafunzi 28
na walio faulu kujiunga na masomo ya shule ya Upili ni wanafunzi saba tu.
Akizungumza kwa
siri kubwa mmoja wa walimu shuleni hapo alisema kuwa inaonesha shule hiyo
baadhi ya walimu wanathamini saana kazi binafi kuliko shughili rasimi na wanayo
itegemea kuendeshea maisha.
‘’Kuna
baadhi ya walimu hawaonekani kazini wiki nzima na bila ya mkuu wa shule kujua
waliko hii inatuathili saana kuendelza shule yetu ambapo muda mwingine
wanashindwa kumaliza maada zote na inatubidi tuwasaidie kufundisha ili kuenda
nao sambamba’’ alisema.
‘’Hohao ndio
wamekuwa kipau mbele katika migomo pindi serikali ikwamapo kutoa masirahi yetu
kwa wakati bila ya kujijaji wao wenyewe
tabia walio nayo ya kutofuata taratibu za shule’’ Aliongeza.
Akijibu
kilio hicho cha wazazi mwalimu mkuu wa shule hiyo Mwampashi Araija kwa njia ya simu alisema kuwa yeye ni
mgeni na shule hiyo nab ado hajaanza kufanya kazi.
Alisema kuwa
wanachosema wananchi huenda ni kweli maana hawawezi kuongea kitu kisicho kuwepo
na kuamua kumsingizia walimu.
‘’Ndio mimi
nimeshalipoti shuleni hapo ila nilipoti mwishoni mwa muhula wa mwisho na
nalijitambulisha kwa walimu wote ila
kujua mwenendo wa mwalimu mmoja mmoja sijajua na kuna baadhi ya walimu siku ya
kulipoti hawakuwepo niliwakuta wachachae’’ alisema Mwampashi.
‘’Kama kuna
matatizo ya aina hiyo naahidi kuya maliza maana tunafanya kazi kwa mujibu wa
sheria bila kufuata sheria zinazo kuongozo hufai kuitwa mwalimu ‘’ alisema
mwampashi.
EmoticonEmoticon