TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 04.12.2014.




·         JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA LYESELO WILAYANI CHUNYA AKIWA NA SILAHA BUNDUKI AINA YA GOBOLE.


·         JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA WANZANI WILAYANI CHUNYA AKIWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU.

KATIKA MSAKO WA KWANZA:

MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA LYESELO WILAYANI CHUNYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA GIBSON MLAWAYA (80) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA SILAHA[BUNDUKI] MOJA AINA YA GOBOLE PAMOJA NA GOLOLI NA BARUTI ZINAZOTUMIKA KATIKA SILAHA HIYO.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 03.12.2014 MAJIRA YA SAA 10:00 ASUBUHI KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA HUKO KATIKA KITONGOJI CHA LYESELO, KATA YA LUPA, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUWINDAJI HARAMU, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.



KATIKA MSAKO WA PILI:

MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA WANZANI WILAYANI CHUNYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA GIBSON MORICE PHILIPO (34) MFANYABIASHARA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE KALI [VIROBA] ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI AINA YA RIDDER PAKETI 10 AKIUZA KATIKA KIBANDA CHAKE.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 03.12.2014 MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA HUKO KATIKA KIJIJI CHA WANZANI, KATA YA MBUYUNI, TARAFA YA SONGWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIZO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUJIMILIKISHA SILAHA KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAFUATE TARATIBU ZA UMILIKAJI WA SILAHA KUPITIA MAMLAKA HUSIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE ANAYEMILIKI SILAHA KINYUME CHA SHERIA ASALIMISHE SILAHA HIYO/HIZO KABLA AJAKAMATWA NA VYOMBO VYA DOLA. PIA ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU KWANI NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.



Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


Previous
Next Post »