Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Profesa Justice Ibrahim
Juma kuwa mwanasheria mkuu wa serikali (AG).
Uteuzi huo umefuatia baada ya aliyekuwa
mwanasheria mkuu Frederick Werema kutangaza kujiuzulu kutokana na
skandali ya mabilioni ya akaunti ya Escrow.
Mapema mwezi huu Rais Jakaya Kikwete pia
alimteua Profesa Juma Assad (CAG) kuwa mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za
serikali baada ya Ludovick Utouh kumaliza muda wake.
EmoticonEmoticon