MSICHANA WA KAZI ALIYETESA MTOTO AKIRI MAKOSA, KUHUKUMIWA JUMATANO DESEMBA 11, 2014

Msichana wa kazi aliyetikisa vyombo vya habari duniani kwa kumtesa mtoto wa miezi 18, Arnella Kamanz aliyekuwa kwenye uangalizi wake huko Uganda, amekiri makosa mbele ya mahaka nchini humo.
Jolly Tumuhiirwe, mwenye umri wa miaka 22, alifanya ukatili uliochukiwa na watu wote Duniani, ambapo alinaswa na camera ya siri, akimtandika mtoto wa mdosi wake kwa kumkanyaga mgongoni akiwa ameanguka chini, kumchapa na kitu kisichojulikana na kumpiga mateke na makofi ya nguvu usoni.
Kitendo hicho kilifuatia mtoto huyo wa kike, kushindwa kula, kutokana na kasi ya ulishwaji ambapo Tumuhiirwe, alikuwa akimlisha mtoto huyo kwa kasi ya ajabu, kwa kushindilia vijiko mdomoni mfululizo.

Huenda mahakama hiyo ikamuhukumu kifungo cha hadi miaka 15 jela, kulipa faini au vyote kwa pamoja. Msichana huyo katika maelezo yake mahakamani, aliomba radhi wazazi wa mtoto huyo, taifa la uganda na walimwengu wote waliokereka na kitendo chake na kuomba msamaha. Hukumu yake itatolewa Jumatano Desemba 11, 2014.

Hata hivyo wakili wa msichana huyo wa kazi aliyekiri kosa hilo Desemba 8, 2014, amedai kuwa mteja wake hakutendewa haki kwa vile hakuelewa mashtaka yaliyokuwa yakimkabili.

Arnella Kamanzi, binti mrembo na mcheshi mwenye umri wa miezi 18 tu, aliyeteswa na Tumuhiirwe
Previous
Next Post »