Watu wa nne wamefariki Dunia na wengine 44 kujeruhiwa kufuatia ajali ya Basi la Abiria la Wibonela



 
Watu wa nne wamefariki Dunia na wengine 44 kujeruhiwa kufuatia ajali ya Basi la Abiria la Wibonela liliokuwa likitokea Kahama Kuja Dar es Salaam kujaribu kulipita gari lililokuwa likifukuzana nalo na Hivyo kumshinda nguvu Dreva na kusababisha ajali katika eneo la Phantom Mkoani Kahama.

Kamanda wa polisi Mkoani kamanda wa Polisi mkoani humo Jastus Kamugisha Amesema Badhi ya Madreva wamekuwa wakiendesha vyombo hivyo vya moto kwa mwendo kasi bila kujua kwamba wamebeba Roho za watu na hivyo kuwasababishia watu ulemavu kwa kuona kwamba niwazoefu katika vyombo hivyo huku wakivunja sheria za usalama Bara Barani.

Kamanda kamugisha amesema kuwa kati ya watu hao wanne walio fariki Dunia watu wazima 3,na mtoto mmoja,ambapo majeruhi wamelazwa kwenye Hospitali ya halimashauri manispaa ya Kahama.

Aidha kwa upande mwingine kamanda amemtaja kijana mmoja Joji Athanasi Dreva Boda Boda mkoani kahama aliyeuawa kwa kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali na kufariki Dunia Baada ya kutaka kuiba fedha na simu wakati akijifanya kutoa Msaada wa kuwaokoa majeruhi kwenye ajali hiyo.

Pia ameongeza kwa kusema kuwa Dreva wa Basi hilo ametoroka hivyo Jeshi la Polisi linamtafuta kujibu sababu za kusababisha ajali hiyo iliyo jeruhi na kupoteza maisha ya watu.
Previous
Next Post »