·
MTOTO WA MIAKA 02 AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA
GARI WILAYANI RUNGWE.
·
WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI.
·
WATU WATATU WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA WAKIWA NA BHANGI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA 02 ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA ANITA BOAZ MKAZI WA KIJIJI CHA MPANDAPANDA ALIFARIKI DUNIA PAPO
HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.730 CKD AINA YA TOYOTA
COASTER LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE HAMPHREY MWALENGO.
AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 16.11.2014 MAJIRA YA
SAA 17:45 JIONI HUKO KATIKA SHULE YA SEKONDARI KIPOKE TUKUYU, BARABARA KUU
YA TUKUYU/MBEYA, KATA YA KIWIRA, TARAFA YA TUKUYU, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA
MBEYA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. DEREVA ALIKIMBIA NA KULITELEKEZA GARI
ENEO LA TUKIO MARA BAADA YA AJALI, JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA
MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N. MASAKI
ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI
PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI
ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA, ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI
ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI [DEREVA] AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI
AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
TAARIFA ZA MISAKO:
KATIKA MSAKO WA KWANZA, WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. SUZANA
JORAM (34) NA 2. PODENSIANA ANDREA (32) WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA UPENDO WANASHIKILIWA
NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO
WA LITA 15.
WATUHUMIWA HAO KWA PAMOJA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 16.11.2014 MAJIRA YA SAA 15:00 ALASIRI HUKO KATIKA KIJIJI
CHA UPENDO, KATA YA MAMBA, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA
MBEYA. WATUHUMIWA NI WAPIKAJI NA WAUZAJI WA POMBE HIYO, TARATIBU ZA KUWAFIKISHA
MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KATIKA MSAKO WA PILI, WATU WATATU WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. JOSHUA
FRANSIS (22) 2. ISSA JUMA (22) 3. EMANUEL MWIGOSO (24) WOTE WAKAZI WA
UYOLE JIJINI MBEYA WANASHIKILIWA NA
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA
NA BHANGI KETE SITA [06] SAWA NA
UZITO WA GRAM 30.
WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 16.11.2014 MAJIRA YA SAA
14:30 MCHANA HUKO KATIKA ENEO LA UYOLE, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA,
JIJI NA MKOA WA MBEYA. WATUHUMIWA NI WATUMIAJI WA BHANGI HIYO, TARATIBU ZA
KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA
MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA
ZA KULEVYA [BHANGI] PAMOJA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME
CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Imetolewa na kusainiwa na:
[BARAKAEL N.
MASAKI – ACP]
KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon