TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA
WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 10.11.2014.
Ø MTOTO
MMOJA AFARIKI DUNIA NA MAMA YAKE
KUJERUHIWA KUFUATIA AJALI YA GARI KUWAGONGANA WATEMBEA KWA MIGUU JIJINI MBEYA.
Ø
JESHI LA
POLISI LINAWASHILIA WATU WANNE KWA KUKAMATWA NA NYARA ZA SERIKALI KATIKA MATUKIO MANNE TOFAUTI WILAYA CHUNYA.
TUKIO
LA KWANZA.
MTOTO MMOJA AFARIKI DUNIA NA MAMA YAKE KUJERUHIWA KUFUATIA AJALI YA GARI
KUWAGONGANA WATEMBEA KWA MIGUU JIJINI
MBEYA
MTOTO MMOJA AITWAE MATHEW KINYUNYU [2], MKAZI WA NJOMBE, ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO NA
MAMA YAKE MZAZI BINTI KIHAKA [41], ALIJERUHIWA
KATIKA AJALI YA GARI KUWAGONGA WATEMBEA KWA MIGUU.
TUKIO HILO LIEMTOKEA TAREHE 09.11.2014 MAJIRA YA SAA 07:30HRS KATIKA ENEO LA IGAWILO-KATA YA IGAWILO, TARAFA
YA IYUNGA JIJI NA MKOA WA MBEYA,
BARABARA KUU YA MBEYA/TUKUYU, KUFUATIA AJALI ILIYOHUSISHA GARI T.486 CGD AINA YA MITSUBISHI FUSO LILILOKUWA
LIKIENDESHWA NA DEREVA MICHAEL BENARD
NYIVUHA [26], MKAZI WA SIMIKE – MBEYA. MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA TARATIBU
ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA
NA WATUMIAJI WENGINE WA VYOMBO VYA MOTO KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO HIVYO
IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA
AJALI ZINAZOEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI
ALIPO DEREVA HUYO AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE
MKONDO WAKE VINGINEVYO AJISALIMISHE MARA MOJA.
TAARIFA
ZA MISAKO
JESHI
LA POLISI LINAWASHILIA WATU WANNE KWA
KUKAMATWA NA SILAHA PAMOJA NA NYARA ZA SERIKALI KATIKA MATUKIO MANNE TOFAUTI
WILAYANI CHUNYA.
KATIKA TUKIO LA KWANZA JESHI LA POLISI LINAMSHIKILIA AMOS
JAMES [29], MKAZI WA KIJIJI CHA MACHINJIONI AKIWA NA SILAHA
/BUNDUKI AINA YA GOBOLE PAMOJA NA NYARA ZA SERIKALI NYAMA YA MNYAMA INSHA YENYE
UZITO WA KILO 2.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 06.11.2014 MAJIRA YA SAA 13:50HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA
MACHINJIONI,KATA YA MAKONGOLOSI,TARAFA YA KWIMBA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA
MBEYA. MTUHUMIWA NI MUWINDAJI HARAMU. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE
MAHAKAMANI.
KATIKA TUKIO LA PILI JESHI
LA POLISI LINAMSHIKILIA ISRAEL
MSANGAWALE [45], MKAZI WA KIJIJI CHA STAMIKO, AKIWA NA NYARA ZA SERIKALI
NGOZI MOJA YA TANDALA, NGOZI MOJA YA
KALUNGUYEYE, NGOZI MOJA YA NGURUWE PORI, JINO MOJA LA NGIRI, PEMBE MBILI ZA
DIGIDIGI NA PEMBE MBILI ZA INSHA.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 06.11.2014 MAJIRA YA SAA 17:50HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA STAMIKO, KIJIJI NA KATA YA MKOLA, TARAFA
YA KIWANJA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUWINDAJI HARAMU. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.
KATIKA TUKIO LA TATU JESHI
LA POLISI LINAMSHIKILIA LUGEDEJA
MAGUTA [45], MKAZI WA KIJIJI CHA LUALAJE, AKIWA NA NYARA ZA
SERIKALI NYAMA YA PONGO KILO 5.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 08.11.2014 MAJIRA YA SAA 08:00HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA NKWANGU, KIJIJI NA KATA YA LUALAJE TARAFA
YA KIPEMBAWE WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA, KUFUATIA MSAKO ULIOFANYWA NA
ASKARI WA WANAYAMA PORI WA PORI LA LUNGWA. MTUHUMIWA NI MUWINDAJI HARAMU. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.
KATIKA TUKIO LA NNE JESHI
LA POLISI LINAMSHIKILIA KANGAI
MASHISHANGA [31], MKAZI WA KIJIJI CHA LUALAJE, AKIWA NA NYARA ZA SERIKALI
GAMBA MOJA LA KOBE,NGOZI MOJA YA MBUZI MAWE, MANYOYA YA NDEGE AINA YA TUMBUSI, MKIA
NA NGOZI YA NGIRI, VICHWA VIWILI VYA NYOKA AINA YA KOBOKO, MIFUPA YA TEMBO, KICHWA
CHA NYOKA AINA YA CHATU,SIKIO LA SIMBA NA FUVU LA NYATI.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 08.11.2014 MAJIRA YA SAA 09:50HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA NKWANGU, KIJIJI NA KATA YA LUALAJE TARAFA
YA KIPEMBAWE WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA, KUFUATIA MSAKO ULIOFANYWA NA
ASKARI WA WANAYAMA PORI WA PORI LA LUNGWA. MTUHUMIWA NI MGANGA WA KIENYEJI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MTU,
KIKUNDI AU MTANDAO WA WANAOJIHUSISHA NA UWINDAJI HARAMU IKIWA NI PAMOJA NA
KUMILIKI SILAHA ISIVYO HALALI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA
KISHERIA DHIDI YAO ZIWEZE KUCHUKULIWA MARA MOJA.
Imetolewa na;
[ AHMED Z. MSANGI – SACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon