Dk. Munroe akiwa nchini Tanzania mwezi Oktoba mwaka huu.
KIONGOZI wa Bahamas Faith Ministries, Dk.
Myles Munroe, mkewe Ruth na watu wengine saba wamefariki dunia katika
ajali ya ndege jana huko Bahamas.
Katika ajali hiyo, ndege ndogo waliyokuwa
wakisafiria iligonga winchi na kulipuka wakati ikiwasili katika Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Grand Bahama.
Dk. Munroe ambaye pia alikuwa mzungumzaji
maarufu wa mambo ya uongozi na biashara duniani, Oktoba 21, mwaka huu
alitoa somo kwa viongozi mbalimbali nchini katika mkutano wake mkubwa
uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar.
Katika mkutano huo, Dk. Munroe kutoka
Nassau, Bahamas, alifundisha mbinu za kuwafanya viongozi waweze
kuchanganua mambo, kutimiza majukumu yao na hatimaye kufikia malengo
makubwa ya kimafanikio ambayo yanaweza kuifanya nchi ipige hatua.
Dr. Myles
Munroe amefariki akiwa na miaka 60 huku akiwa kwenye ndoa na mkewe kwa
miaka 35 Ajali ya ndege hiyo inayosemekana ilikua na watu wengine 9
akiwemo Makamu wa Rais wa Bahamas Faith Ministries, mchungaji Richard
Pinder watu wengine haijajulikana bado majina yao japo inasemekana
alikuwemo mtoto wa kike wa Dr. Myles Munroe ndani ya ndege hiyo.
EmoticonEmoticon