Adebayor adai mamaake ni mchawi


Mchezaji huyu wa kilabu ya Totenham amedai kuwa mamaake amekuwa akitumia uchawi kujaribu kumuharibia kazi yake.
Mshambuliaji wa kilabu ya Totenham nchini Uingereza Emmanuel Adebayor amekosana na mamaake kwa madai kwamba anatumia uchawi kumharibia kazi yake.
Duru zimearifu kuwa mama huyo tayari ameondoka katika nyumba ya familia huku dadaake Adebayor akiambia radio moja ya mjini Accra kwamba Adebayor ndiye aliyemfukuza.
Lakini mchezaji huyo wa zamani wa kilabu ya Arsenal anadai kwamba mamaake aliondoka mwenyewe na kwamba hawana mawasiliano yoyote kati yao kwa kuwa amekuwa akitumia uchawi kutaka kumuharibia kazi yake.BBC
Previous
Next Post »