TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 29.09.2014.
·
WATU WATATU WAUAWA KWA KUPIGWA KATIKA MATUKIO
MATATU TOFAUTI MKOANI MBEYA.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA
ALIFAHAMIKA KWA JINA MOJA LA KABOTE (41) MKAZI WA MWANAVALA WILAYANI
MBARALI ALIUAWA KWA KUCHOMWA MIKUKI SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA MTU
MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA NYAMANIENGO
KINANGA AMBAYE NI MMILIKI WA KLABU CHA POMBE ZA KIENYEJI.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 28.09.2014
MAJIRA YA SAA 23:00 USIKU HUKO
KATIKA KLABU CHA POMBE ZA KIENYEJI, KIJIJI CHA MWANAVALA, KATA YA IMALILO
SONGWE, TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA,
CHANZO CHA TUKIO HILO NI BAADA YA MAREHEMU KUSHINDWA KULIPA KIASI CHA TSHS. 500 ALIYOKUWA AKIDAIWA BAADA YA
KUNYWA POMBE KLABUNI HAPO.
WATU 13 WANASHIKIRIWA KWA MAHOJIANO
KUHUSIANA NA TUKIO HILI KWANI BAADA YA MAREHEMU KUSHINDWA KULIPA FEDHA HIYO,
WATU HAO 13 WALIOKUWEPO ENEO HILO WALIANZA KUMKIMBIZA MAREHEMU HUKU WAKIPEGA
KELELE. MSAKO MKALI UNAENDELEA KUWATAFUTA WATUHUMIWA WENGINE WA TUKIO HILI
KWANI WANAFAHAMIKA NA WALIKIMBIA MARA
BAADA YA TUKIO.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE
MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA
HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTU MMOJA
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA AMBUMBULWISYE
MWASOMOLA (35) MUINJILISTI NA
MKAZI WA KIJIJI CHA LUKASI ALIUAWA KWA KUPIGWA NA MCHI WA KUTWANGIA SEHEMU ZA
KICHWANI NA MTU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA SWALAPO
MWAISANILA (56) MKAZI WA KIJIJI
CHA LWANGWA AMBAYE NI MGONJWA WA AKILI.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 27.09.2014
MAJIRA YA SAA 23:30 USIKU HUKO
KATIKA KIJIJI CHA LUKASI, KATA YA LWANGWA, TARAFA YA BUSOKELO, WILAYA YA
RUNGWE, MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA TUKIO HILO NI BAADA YA MAREHEMU AMBAYE NI
MUINJILISTI WA KANISA LA BAPTISTI KUTAKA KUMFANYIA MAOMBI MTUHUMIWA HUYO
KUTOKANA NA UGONJWA WA AKILI ALIOKUWA NAO NA NDIPO MTUHUMIWA ALICHUKUA MCHI NA
KUMPIGA NAO MAREHEMU KICHWANI NA KUPELEKEA KIFO CHAKE. MTUHUMIWA AMEKAMATWA.
KATIKA TUKIO LA TATU:
MTU MMOJA
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA RICHARD NELSON
FWAMBO (50) MKAZI WA UTAMBALILA
WILAYA YA MBARALI ALIUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI SEHEMU ZA
KICHWANI NA MTU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA KHAMIS
MGALA (32) MKAZI WA MLOWO –
MBOZI AMBAYE NI MTOTO WAKE WA KAMBO.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 28.09.2014 MAJIRA
YA SAA 01:00 USIKU HUKO KATIKA
KITONGOJI CHA MAGAMBA, KIJIJI CHA UTAMBALILA, KATA YA NAMBIZO, TARAFA YA ITAKA,
WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA MTUHUMIWA KABLA YA KUTEKELEZA
TUKIO HILO, ALIVUNJA MLANGO NA KUINGIA NDANI NA KUANZA KUMSHAMBULIA MAREHEMU
AMBAYE ALIKUWA AMELALA NDANI YA NYUMBA YAKE AKIWA NA MKE WAKE AITWAYE YUSTINA KASHAPAMBA@NAKAMANGA (40) MKAZI WA UTAMBALILA AMBAYE NI MAMA
MZAZI WA MTUHUMIWA.
CHANZO CHA TUKIO
HILO, INADAIWA KUWA MTUHUMIWA ALIKUWA HATAKI/HAPENDI MAMA YAKE HUYO KUISHI NA
MAREHEMU AMBAYE NI BABA YAKE WA KAMBO BAADA YA BABA YAKE MZAZI KUFARIKI. MWILI
WA MAREHEMU UMEKUTWA NA MAJERAHA MANNE SEHEMU ZA KICHWANI.
AIDHA, INADAIWA
KUWA MTUHUMIWA KWA MUDA MREFU HAKUONEKANA KIJIJINI HAPO LAKINI GHAFLA SIKU MOJA
KABLA YA TUKIO HILO ALIONEKANA. TAARIFA ZA AWALI ZINADAI KUWA, MTUHUMIWA
KIPINDI CHA NYUMA ALIWAHI KUMJERUHI MAMA YAKE PAMOJA NA MAREHEMU. MSAKO MKALI
UNAENDELEA WA KUMTAFUTA MTUHUMIWA KWANI ALIKIMBIA NA KUTOKOMEA KUSIKOJULIKANA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE
MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA
HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon