Asilimia 52 ya Watanzania wanawake kwa wanaume imedaiwa kuwa wanatumia vipodozi ambavyo si salama kwa afya zao na ambavyo matumizi yake yamepigwa marufuku nchini.
Baadhi ya vipodozi vilivyopigwa marufuku kutokana na kusababisha madhara ya kiafya.
Afisa kutoka asasi ya Envirocare Bi. Ephrasia Shayo amesema hayo leo wakati wa kampeni ya kuzuia matumizi ya vipodozi hatari inayoendeshwa na asasi hiyo kwa kushirikiana na Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA.
Bi. Ephrasia ametaja baadhi ya madhara yanayotokana na matumizi ya vipodozi hivyo kuwa ni saratanio ya ngozi, kuzaa watoto wenye ulemavu wa akili, kuharibika kwa mimba, maelezo ambayo yameungwa mkono na muelimishaji umma wa TFDA Bw. James Ndege.
Kwa mujibu wa Ndege, idadi kubwa ya vipodozi hivyo imeingia nchini kwa njia za panya kutokana na hatua zinazochukuliwa na TFDA kudhibiti uingiaji wa vipodozi hivyo katika mipaka.
Amesema watu wengi wanakimbilia kunua vipodozi hivyo kutokana na kuuzwa kwa bei nafuu ambayo kila mwananchi anaweza kuimudu pasipo kujali madhara anayoweza kuyapata.
Muelimishaji huyo kutoka TFDA amewataka wananchi kuchukua tahadhari zote kuepuka matumizi ya vipodozi hatari, kama vile vyenye madini ya zebaki, hydroquinone na nyinginezo ambazo zikiingia mwililini zinaleta madhara makubwa kwenye viungo vya ndani ya mwili.
Artikel Menarik Lainnya
More 1 of 376 TAASISI YA KILIMANJARO DIALOGUE YATAKA WANAHABARI KUTUMIA KALAMU ZAO KUDUMISHA AMANI NCHINI Mdhamini wa Taasisi ya Kilimanjaro Dialogue, Habib Miradji (katikati) akiongoza m
NAFASI ZA KAZI Nafasi za kazi UN kwa watanzania National Consultant – Agricultural Productivity http://ajir
SABODO AMSHAURI RAIS MAGUFULI AZIDI KUPUNGUZA BARAZA LA MAWAZIRI Mfanyabiashara maarufu nchini, Jaffar Sabodo akizungumza nyumbani kwake Upanga Dar es Sa
Nicolas Sarkozy, atangaza kuwania tena urais nchini Ufaransa Rais wa zamani wa Ufaransa , Nicolas Sar
Mazishi ya mpiga picha Mpoki Bukuku yalivyofanyika kijijini kwao Dodoma Mamia ya wadau pamoja na wale wa Tasnia ya Habari wameendelea kujitokeza kwa wingi katika ma
RC SHIGELLA AWATAKA WENYEVITI WA MITAA KUSIMAMIA KWA UMAKINI SHUGHULI ZA MAENDELEO KWENYE MAENEO YAO Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mh Martini Shigella akizungumza na wenyeviti wa mitaa kuhusu kujadil
EmoticonEmoticon