TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 18.09.2014.



·         MWENDESHA PIKIPIKI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI JIJINI MBEYA.


·         JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATATU KWA TUHUMA MBALIMBALI.



KATIKA TUKIO LA KWANZA:

MWENDESHA PIKIPIKI AMBAYE HAKUWEZA KUFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE MARA MOJA, JINSI YA KIUME, UMRI KATI YA MIAKA 18 – 23 AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI ISIYOFAHAMIKA IKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFHAMIKA.

AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 17.09.2014 MAJIRA YA SAA 20:50 USIKU HUKO NJIA PANDA YA MOONDUST, KATA YA RUANDA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. DEREVA WA GARI ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO NA JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA NA WATUMIAJI WENGINE WA VYOMBO VYA MOTO KUWA MAKINI, KUZINGATIA NA KUFAUATA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI. AIDHA, ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA [DEREVA] AZITOE KWENYE MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.

TAARIFA ZA MISAKO:

KATIKA MSAKO WA KWANZA ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 16.09.2014 MAJIRA YA SAA 10:00 ASUBUHI HUKO KATIKA MAENEO YA MWAKIBETE, KATA YA MWAKIBETE, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA.

MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA EVA KIHUNGU (27) MKAZI WA MWAKIBETE ALIKAMATWA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI UJAZO WA LITA MOJA [01]. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIYO.

KATIKA MSAKO WA PILI, MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA IKUPA ALLY (25) MKAZI WA MWAKIBETE ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI UJAZO WA LITA SITA [06].

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 17.09.2014 MAJIRA YA SAA 12:30 MCHANA HUKO MAENEO YA JUA KALI, KATA YA JUA KALI, TARAFA YA BONDE LA USONGWE, JIJI NA MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MTUMIAJI WA POMBE HIYO.

AIDHA KATIKA MSAKO WA TATU ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 16.09.2014 MAJIRA YA SAA 10:30 ASUBUHI HUKO MAENEO YA MWAKIBETE, KATA YA MWAKIBETE, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA.

MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA AMONI MWAIKOBA (21) MKAZI WA MAMA JOHN ALIKAMATWA AKIWA NA BHANGI KETE 12 SAWA NA UZITO WA GRAMU 60. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MTUMIAJI WA BHANGI HIYO.

TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA ZINAENDELEA KUFANYIKA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA PAMOJA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA, ANAENDELEA KUTOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ZA MTU/WATU AU MTANDAO WA WATU WANAOJIHUSISHA NA UTENGENEZAJI NA UUZAJI WA POMBE YA MOSHI PAMOJA NA BHANGI ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKUE MKONDO WAKE.

                         Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Previous
Next Post »