Walimu wote waliopelekwa na serikali katika shule ya msingi ya Endeshi iliyoko kijiji cha matala kata ya barai wilayani Karatu mkoani Arusha wameacha kazi na kutorokea kusikojulikana na kumuacha mkuu wa shule peke yake kwa kile kilichodaiwa kuwa ni mazingira magumu ya eneo hilo.
Mkuu wa shule hiyo Bw Pilemon Amsi amesema tatizo kubwa ni kukosekana kwa mahitaji muhimu zikiwemo nyumba za walimu na kwamba amebaki peke yake hali inayomfanya ashindwe kutoa huduma ,na hali inaendelea kuwa mbaya kwani wanafunzi nao wanaendelea kutoroka.
Afisa mtendaaji wa kijiji hicho Bw, Gitoyanga Gweku amesema pamoja na tatizo la ugumu wa mazingira walimu wanaopelekwa kwenye shule hiyo ni wale waliokata tamaa na walioshindikana kwenye maeneo mengine.
Nao badhi ya wazazi wamesema hawaoni sababu ya kuwalazimisha watoto wao kwenda shule ambayo haina walimu kwani ni kupoteza muda na kwamba ni bora wafanye kazi zingine ikiwemo ya kuchunga mifugo.
Mkuu wa wilaya ya karatu Bw Felexs Ntebenda ametembelea shule hiyo na kujionea hali halisi na amesema serikali itawatafuta walimu waliotoroka popote walipo kwani hata kama kulikuwa na tatizo ufumbuzi wake sio kutoroka na kuwatelekeza wanafunzi.
EmoticonEmoticon